Na Lusajo Frank, DSJ 

WAMAREKANI wamepiga kura kumchagua Rais katika uchaguzi ulioligawanya taifa hilo kwa kiwango kisichokuwa na kifani kwa mwaka huu ambapo uchaguzi huo matokeo yameanza kutangazwa.

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Mgombea wa Kiti cha Urais,Biden ameshinda kwenye majimbo ya Virginia, Delaware,Vermont Connecticut, Illinois, Maryland, Massachusetts, New Jersey na Rhode Island huku Trump akiyanyakua majimbo la Virginia magharibi, Kentucky, na South Carolina, Alabama, Mississippi, Oklahoma na Tennessee.

Mpaka sasa Joe Biden anaongoza kwa kura za wajumbe maalum 238 na Mgombea Trump akiwa na idadi ya kura 213 wajumbe maalum.

Matokeo yanaendelea kutangazwa, wamarekani zaidi ya milioni mia moja wamepiga kura ya kuamua iwapo watamrudisha madarakani  Donald Trump au wataamua kuleta mabadiliko kwa kumchagua mgombea wa chama cha Democratic, Joe Biden baada ya wanasiasa hao wawili kupambana vikali kwenye kampeni zao katika muktadha wa janga la  maambukizi ya virusi vya corona.

Idadi hiyo inaashiria kwamba ushiriki wa wapiga kura utavunja rekodi ya karne katika uchaguzi wa mwaka huu

Kura za maoni zinaonyesha kuwa mgombea Biden yuko mbele lakini kinyang'anyiro kinakwenda bega kwa bega katika majimbo yanayoweza kuamua mshindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...