
Mwenyekiti wa Jumuia ya
Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari jijini Dodoma, kumshukuru Mungu kwa Uchaguzi Mkuu wa
Tanzania kufanyika kwa amani na utulivu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa
Jumuia hiyo, Askofu Oswald Mlay na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa
Dodoma, Askofu Evance Chande. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
…………………………………………………………………….
Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma.
MWENYEKITI
wa Tume ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salumu amewasihi
watanzania kuendelea kumshukuru Mungu kwa wema aliowatendea baada ya
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa salama na amani.
Ameyazungumza
hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, akiwa
pamoja na wajumbe wa tume ya kitaifa ya maridhiano na wa mkoa wa Dodoma.
Aidha,
Sheikh Alhad Mussa amesema kuwa inatakiwa sasa baada ya uchaguzi
kumalizika salama ni kuungana kuendelea kuiombea kwa Mungu serikali
iliyoshinda iongoze vema.
“Tunashukuru
Mungu Uchaguzi umeisha kwa amani na salama, kilicho mbele yetu ni
kuungana kuendelea kuiombea Mungu Serikali iliyopo madarakani ituongoze
salama.
Katika
chaguzi zote kuna kushinda na kushindwa, huwezi kukubalika na kila
mmoja haiwezekani, manabii wa Mwenyezi Mungu na hata Wacha Mungu
hawakukubalika nao walipingwa, hii ni desturi ni jambo la
kawaida,”amesema Sheikh Alhad.
Ameshauri
upande ambao haujaridhika usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu
zilizopo ikiwemo ya kisheria na hata jumuia hiyo inaweza kuweka mambo
sawa.
“Kubwa
tunawaomba Watanzania Nchi yetu iendelee kuwa salama na utulivu,
tunahitaji nchi yenye amani ili tuweze kufanya shughuli zetu kwa
ukamilifu bila bughudha yoyote, tusijaribu kuchezea amani iliyopo,
tutajuta, tuna mifano mingi ya nchi mbalimbali zilizochezea amani,
kuirejesha ni ngumu sana.”
Amesema
viongozi wa Dini walimlilia sana Mungu ili Uchaguzi uvuke kwa salama na
amani, hivyo inabidi kumshukuru Mungu kwa wema wake aliotutendea. na
kwamba wakifanya hivyo Mungu atatuzidishia.
Alimalizia
kwa kutoa shukrani kwa viongozi wote walioiombea kwa Mungu nchi wakati
wa mlipuko wa ugonjwa wa corona na Uchaguzi Mkuu na sasa iko salama
hivyo tuendelee kumshukuru Mungu naye ataendelea kutusikiliza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...