Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akiwasilisha mada katika Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya ushirikiano katika siasa, ulinzi na Usalama unaondelea Mjini Gaborone, Botswana.


Na Mwandishi wetu, Gaborone

MAKATIBU Wakuu wa SADC -TROIKA wamekutana na kujadiliana Mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ndani ya SADC mjini Gaborone, Botswana.

Awali, Mkutano wa Makatibu Wakuu ulifunguliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana, Bw. Gaeimelwe Goitsemang ambae pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.

Ni mara ya kwanza kwa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC) kukutana ana kwa ana tangu ulipotokea ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (Covid-19).

Kwa upande wa Makatibu wakuu waliohudhuria katika Mkutano huo kutoka Tanzania ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe.

Mkutano wa Makatibu Wakuu utafuatiwa na Mkutano wa dharua wa baraza la Mawaziri wa asasi ya SADC ya ushirikiano katika siasa, ulinzi na usalama baadae leo mchana mjini Gaborone.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...