Meneja Wa Kanda Crdb Bw.Lusingi Sita Akitoa Neno La Ufunguzi Katika Jukwaa La Kongamano La Wanawake Jijini Mwanza

Mkuu Wa Mkoa Wa Mwanza Bw. John Mongella Akihutubia Washiriki Kwa Ajili Ya Ufunguzi Wa Jukwaa La Kongamano Maalum La Wanawake Liliandaliwa Na Benk Ya Crdb Jijini Mwanza

=======  ======== ========


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza awataka wanawake kuchangamkia fursa za CRDB Malkia


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa kongamano la uwezeshaji wanawake mkoa wa Mwanza ili kuonyesha fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wanawake. Akifungua kongamano hilo Mongela ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa kongamano hilo huku akiwataka wanawake kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki hiyo kupitia CRDB Malkia.

Mongela aliipongeza Benki ya CRDB kwa hatua ambayo imechukua hivi karibuni ya kupunguza riba ya mikopo inayotolewa kwa wanawake wajasiriamali kutoka asilimia 24 hadi asilimia 14. Akitoa hotuba yake katika kongamano hilo lililohudhuriwa na wanawake wajasiriamali zaidi ya 300, Mongela alisema hatua ya Benki ya CRDB kupunguza riba kwa kutoka asilimia 24 iliyokuwa ikitozwa mwanzo hadi asilimia 14 itasaidia wanawake wengi zaidi kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo.

“Kupungua kwa riba ina maana inapunguza mzigo mkubwa wa marejesho kwa wanawake na kuwafanya kuwa na fedha nyingi kwa ajili ya uwekezaji katika biashara zao na hivyo kupelekea kufanikisha zaidi,” alisema Mongela.

Mongela alisema pamoja na tafiti kuonyesha wanawake wamekuwa na ushiriki mkubwa katika shughuli za uchumi nchini, kwa asilimia 54, ni asilimia 60% tu ya wanawake ndio wenye kufikiwa na huduma rasmi za kifedha.

“Niwapongeze pia kwa kuboresha masharti ya dhamana ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kuweza mikopo,” aliongezea Mongela huku akiwataka wanawake pia wajitokeze kwa wingi kufungua akaunti ya Malkia itakayosaidia kufanikisha malengo yao kwa kujiwekea akiba kidogokidogo jambo litakalosaidia kujenga imani kwa taasisi za fedha.

Mongela alisema jitihada hizo zinazofanywa na Benki ya CRDB katika uwezeshaji wa makundi mbalimbali ya wananchi zimekuwa na msaada mkubwa katika kuisaidia Tanzania kufikia lengo la kuwa nchi yenye uchumi wa kati.

“Azma ya Serikali ni kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara kwa wanawake ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii,” alisema Mongela.

Naye Mbunge wa Ilemela, Mheshimiwa Angelina Mabula aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma ya Malkia Rafiki katika matawi yake akisema kuwa huduma hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kotoa elimu ya fedha kwa wanawake na usaidizi wa kutosha katika huduma ya CRDB Malkia. Benki ya CRDB imeweka wataalamu wa uwezeshaji wanawake wajulikanao kama “Malkia Rafiki” katika mtandao wa matawi yake yote nchi nzima.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa Manunuzi wa Benki ya CRDB, Pendason Philemon alisema huduma ya CRDB Malkia imelenga katika kumtambua, kumpa nafasi na kumuwezesha mwanamke wa Kitanzania kufikia malengo yake kupitia mikopo ya biashara na ujasiriamali, kujiwekea akiba kwa akaunti ya Malkia na mafunzo ya uendeshaji biashara.

“Mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi June mwaka huu, Benki yetu tayari ilikuwa imekwisha toa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 600 kwa wanawake zaidi ya elfu 55,” alisema Pendason huku akibainisha kuwa zaidi ya wanawake 30,000 tayari wameshajiunga na akaunti ya Malkia.

Mkuu Wa Mkoa Wa Mwanza Watano Kutoka Kulia Akiwa Katika Picha Ya Pamoja Na Viongozi Wa Benki Ya Crdb Na Baadhi Ya Washiriki Mara Baada Ya Kufungua Jukwaa La Kongamano Maalum La Wanawake Jijini Mwanza

Pendason alisema pamoja na mafanikio ambayo Benki ya CRDB imeyapata katika kumuwezesha mwanamke, bado idadi ndogo ya wanawake wamekuwa wakijitokeza kupata huduma kutokana na changamoto ya riba, masharti magumu ya dhamana na kukosa uelewa wa huduma za kifedha.

“Tukiwa Benki ya kizalendo inayothamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa letu, tukasema ni vyema tukatafuta suluhisho la changamoto hizi ili kuweza kumsaidia mwanamke kufankisha malengo yake zaidi.

Baadhi Ya Washiriki Ambao Wamejitokeza Katika Jukwaa La Kongamano Maalum La Wanawake Lililoandaliwa Na Benki Ya Crdb Jijini Mwanza

Pendason alisema CRDB Malkia sasa hivi inawawezesha wanawake kupata mikopo kwa riba ndogo ya asilimia 14 kulinganisha na asilimia 24 iliyokuwa ikitozwa mwanzo huku masharti ya upatikanaji wa mikopo yakirahisishwa kwa kiasi kikubwa.

“Kupungua kwa riba kuna maana wanawake sasa wanaweza kukopa zaidi na kwa gharama nafuu kulinganisha na mwanzo hivyo kusaidia kufanikisha malengo yao kwa uharaka zaidi,” alisema Pendason.


Akihitimisha kongamano hilo, Pendason alisema, Benki ya CRDB imejipanga vilivyo kushiriki katika safari ya mafanikio ya wanawake wote wa Tanzania na kuwaomba wanawake wajitokeze kwa wingi katika matawi ya Benki ya CRDB ili kuanza kufurahia huduma hiyo mpya ya CRDB Malkia. “Ukifika tawini ulizia Malkia Rafiki naye atakusaidia kuanza safari yako ya mafanikio,” alihitimisha Pendason.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...