Mdau wa Elimu na Maendeleo David Kayuni akizungumza na wanafunzi na  Walimu wa Shule ya Sekondari Ukwamani alipokwenda kutoa msaada wa komputa katika shule hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Ukwamani Saphina Egha akizungumza kuhusiana namna walivyopokea msaada wa komputa.

Mdau wa Elimu na Maendeleo David Kayuni akimkabidhi komputa mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Ukwamani Saphina Egha jijini Dar es Salaam.
 
 
Mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ukwamani Khadija Selemani akitoa shukurani kwa wanafunzi wenzake mara baada ya kukabidhiwa komputa katika shule hiyo.
 
******************
 
Na Amir Atick,  Michuzi Tv Mdau wa elimu na Maendeleo David Kayuni amekabidhi komputa Tano (5) katika shule ya Sekondari  Ukwamani-Kawe Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam zenye thamani ya Sh.3.2.

Akizungumza Mara baada ya kukabidhi komputa hizo Kayuni amesema kuwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inakuwa kwa kasi hivyo wanafunzi wanatakiwa kujua Teknolojia mapema kabla hawajafika hawajafika katika elimu ya juu.

Amesema kuwa wanafunzi  wa Sekondari wakipata mwanga wa Tehama wakati wakiwa Sekondari   watakuwa wanafunzi wenye uwezo katika elimu ya Sekondari na vyuo.

"Ninaamini komputa hizi mtazituza ikiwa ni pamoja na kuzitumia katika masomo na mtumie kwa usalama zaidi kwani msipotumia kwa usalama zinaweza kuwapotosha hasa katika masuala ya wa data 'Internet'"amesema Kayuni.

Aidha amesema kuwa licha ya kutoa komputa hizo ataendelea kuwa na ukaribu wa shule hiyo katika kusukama gurudumu la elimu kwenda mbele zaidi na kuongeza kuwa nchi imeingia katika uchumi wa kati hivyo kunahitaji kuwa na wataalam wa kuweza kwenda na uchumi huo.

Amesema serikali imewekwa mikakati ya kuboresha elimu hivyo Kama wadau hatutakiwi kuwa nyuma katika kwenda na serikali kwa kuunga mkono.
Nae Mkuu wa Shule ya Sekondari Ukwamani Mkuu wa shule  Saphina Egha amesema anawakaribisha wadau wengine  wa elimu na maendeleo kuleta misaada mbalimbali itakayo wanafunzi katika kujifunza na kutimiza ndoto zao hapo mbeleni.

Amesema kuwa komputa kwa sasa zinahitajika kwani dunia inatoka katika mfumo wa karatasi na kuingia kutumia komputa.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...