BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limewafutia matokeo watahiniwa 1,059 kutoka shule 38 zilizofanya udanganyifu katika mitihani ya kuhitimu darasa la saba mwaka huu.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi, Novemba 21, 2020 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde, amesema watahiniwa hao hawatapata nafasi nyingine ya kurudia mitihani hiyo.

Alisema pamoja na kamati ya mitihani kutimiza wajibu wao vizuri, kulijitokeza matukio machache ya udanganyifu wa mitihani katika baadhi ya shule nchini.

“Jumla ya shule 38 sawa na asilimia 0.22 ya shule zote za msingi 17,329 zilizofanya mitihani, zimebainika kufanya udanganyifu wa mitihani kwa namna mbalimbali. Watahiniwa 1,059 sawa na asilimia 0.1 ya wote 1,023,950 waliofanya mitihani walibainika kudanganya.” Amesema.

Ameongeza kwamba shule hizo zilifanya makosa mbalimbali ikiwamo kuiba mitihani, kugawa majibu kwa wanafunzi na kubadilisha watahiniwa kwa kuwaweka wasio halisi kuwafanyia mitihani wanafunzi watoto.

Shule zilizobainika kufanya udanganyifu huo ni pamoja na Ngiloli, Nguyami, Ibuti, Ihenje, Bwawani, Mogohigwa, Chakwale, Msingisi zilizopo Halmashauri ya Gairo.

Zingine ni Mafiri, Kibogoji, Ng’wambe, Digalama, Dihinda kutoka Halmashauri ya Mvomero na shule za msingi za Nyawa A iliyopo Halmashauri ya Bariadi vijijini (Simiyu).

Shule zingine ni za Halmashauri ya Chabutwa, Sikonge Tabora ikiwemo shule ya msingi Chabutwa, Usagari, Uyui Tabora Siashimbwe iliyopo Moshi Kilimanjaro, Dominion Arusha, Matogoro ya Tandahimba Mtwara, Ng’arita Bariadi Vijijini mkoani Simiyu, Olkitikiti Kiteto iliyopo Manyara na Nyamimina Buchosa, Mwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...