Na. Vero Ignatus ,Arusha.

Naibu Gavana wa Benki kuu Tanzania (BOT) Dr.Yamungu Kayandabila amekipongeza Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA) kwa kusambaza pembejeo bora kwa Wakulima hivyo kuongeza uzalishaji na kusaidia upatikanaji wa malighafi katika viwanda .

Akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA),Naibu Gavana amekitaka chama hicho kuendelea kushirikiana na taasisi za fedha katika kukuza kilimo ili kuinua pato la mkulima na taifa kwa ujumla.

Dr.Yamungu amesema kuwa katika safari ya uchumi wa viwanda wakulima ni wadau muhimu ambao wanapaswa kuhakikisha kuwa wanazalisha malighafi kwa wingi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TFA, Peter Sirikwa amesema kuwa walainza kusambaza pembejeo kwa wanachama wao na wanampango wa kuwafikia wanachama 5000 na wakulima walioko nje ya chama hicho.

“Tunaomba serikali itasaidia kuweka mazingira mazuri ya uagizaji wa pembejeo kutoka nje ili wakulima wetu wapate pembejeo bora na kwa gharama nafuu” Alisema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Peter Sirikwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa TFA, Jastin Shirima amesema kuwa mpango wao ni kuwafikia wakulima wengi na kusambaza pembejeo ambapo kwa sasa wana vituo 17 nchini vya kusambaza pembejeo.

Kwa upande Wake Mkulima aliyehudhuria Mkutano huo Anselim Antony ameipongeza TFA kwa mpango huo kwani utawawezesha wakulima kuondokana na pembejeo feki.




Naibu Gavana wa Benki kuu Tanzania (BOT) Dr.Yamungu Kayandabila akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TFA, Peter Sirikwa akitoa taarifa yake katika Mkutano Mkuu wa TFA






5.Wanachama wa TFA wakifuatilia kwa makini mkutano

7.Wakwanza kushoto ni 2..Naibu Gavana wa Benki kuu Tanzania (BOT) Dr.Yamungu Kayandabila akiwasili katika ukumbi wa Mkutano Mkuu wa TFA,Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa TFA ,Jastin Shirima .

Picha ya Pamoja ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wapili kutoka kulia ,akiwa na bodi ya TFA.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...