Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wakulima wa zao la parachichi mkoani
Njombe wanaiomba serikali kuboresha ghalama za pembejeo hususani
zinazotumika katika kilimo hicho,ili kuwasaidia wakulima na kunufaika na
kilimo hicho ambacho kinaendelea kukuwa kukua kwa kasi katika maeneo ya
mkoa wa Njombe.
Elijius Wela ni mkulima wa parachichi na
mkurugezni wa kampuni ya MADEBE inayoshughulika na upandaji wa
parachichi kutoka kwenye kitalu kwenda shambani,akizungumza na vyombo
vya habari shambani kwake amesema wakulima wengi kwao changamoto ni
ghalama ya Pembejeo,wanaomba serikali kushusha bei ya Pembejeo pamoja na
kuweka ruzuku ya kutosha ili zao hili liendelee kukua na kukuza zaidi
uchumi wa Njombe na taifa kwa ujumla.
"Serikali ikazane kuangalia
pembejeo za zao la parachichi iwe chini na waweke ruzuku ya kutosha ili
kuleta unaafuu kwa wakulima"alisema Wela.
Amesema wananchi wamehamasika kuingia katika zao hilo kutokana uzuri kibiashara na kuwasadia wengi kufanikiwa kiuchumi.
"Kwa
kweli parachichi inalipa kwasababu mkulima akifanikiwa kupanda shamba
Ekari moja na miti ikitimiza mika 7 na kuhudumia vizuri hawezi kukosa
milioni ishirini na atafanikiwa sana na tunashukuru serikali
inavyotuuunga mkono kwa kuwa inatupatia zao ambalo lipo soko kidunia,na
tuna uwezo Zao hilo litatupeleka mbali mkoa wa Njombe Kiuchumi"Aliongeza
Wella
Baraka Muyamba na Jiskaka Mwalyego ni baadhi ya watumishi
wanaofanya kazi katika kitalu cha uzalishaji wa parachichi kilichopo
kijiji cha Kifanya halmashauri ya mji wa Njombe kinachomilikiwa na bwana
MADEBE,wanasema licha ya kufanya kazi katika kampuni hiyo lakini
wamehamasika kuingia katika kilimo kutokana faida inayotokana na zao
hilo.
"Kwanza kampuni hii imekuwa msaada mkubwa kwa kupata ajira
inayotusaidia kukidhi mahitaji,na mimi nimehamasika kwenye kilimo hiki
lakini bado tunaendeleea kupata elimu zaidi ili tuweze kunufaika"Alisema
Baraka Muyamba
"Mimi nipo nafanya kazi hapa ya Grafting,na kwa
kweli kwa mkoa wa Njombe parachichi linakubali na lina faida na kwa
kuhamasika kwangu tayari Mbeya nina shamba Ekari 60 amabyo yanaandaliwa
na mengine ni mapori kwa ajiri ya kwenda kuanza kilimo cha
Parachichi"alisema Jiskaka Mwalyego
Sadam Fundikila ni meneja wa
kampuni ya MAKE A FOREST DEVELOP BEST COMPANY LTD (MADEBE) amesema
kampuni hiyo inayohusika na utoaji wa huduma mbali mbali za kilimo
hususani Parachichi,wamekuwa na msaada kwa jamii hususani kijiji cha
Kifanya kwa kufanikiwa kuajili vijana 200 wanaolipwa kwa kazi na 5
wakilipwa kwa mwezi huku pia wakiendelea kutafuta masoko ya zao la
parachichi kwa wakulima.
"Lakini pia tumeanzisha mpango wa kuwa
na kikundi kwa wakulima kitakachojihusiha na uzalishaji wa
parachcichi,licha ya kuendelea kuhusika na utoaji wa huduma za kilimo
kwenye mazao ya misitu na matunda kwa maana ya parachichi"alisema bwana
Fundikila
Jiskaka Mwalyego akiendelea na zoezi la Grafting katika kitalu cha miche ya Parachichi ya bwana MADEBE mjini Njombe.
Eneo la Kitalu cha miche ya parachichi iliyostawi inayomilikwa kampuni ya MADEBE eneo la kifanya halmashauri ya mji wa Njombe ikionekana baada ya kupigwa picha




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...