Waziri
Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa leo Novemba 8, 2020 amemtembelea na
kumjulia hali mwanamziki mkongwe nchini Kikumbi Mwanza Mpango maarufu
kama King Kikii, Nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ally, Jijini Dar es
Salaam.
Mhe.
Majaliwa alimpa pole Kinkii anayesumbuliwa na matatizo ya Mgongo na
amemtakia pona ya haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake kama
kawaida.
Aidha,
Mhe. Majaliwa pia alimjulia hali Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rechal Kasanda
ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu baada
ya kupata ajali ya gari Wilayani Mlele, Mkoani Katavi alipokuwa kwenye
ziara ya kikazi.
Akizungumza na Mhe. Kasanda, Mhe. Majaliwa alimtakia pona ya haraka ili aendelee na majukumu yake ya kuwatumikia WanaKatavi.
Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akimpa pole Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rechal Kasanda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari Wilayani Mlele, Mkoani Katavi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi, Novemba 8, 2020. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera. Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama (King Kiki) , anayesumbuliwa na matatizo ya pingiri za mgongo, nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ali, Novemba 8, 2020.
Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Msanii mkongwe wa
muziki wa dansi Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama (King Kiki) ,
wakati alipomjulia hali msanii huyo anayesumbuliwa na matatizo ya
pingiri za mgongo, nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ali, Novemba 8, 2020.
Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akimpa pole Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rechal Kasanda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari Wilayani Mlele, Mkoani Katavi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi, Novemba 8, 2020. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera. Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama (King Kiki) , anayesumbuliwa na matatizo ya pingiri za mgongo, nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ali, Novemba 8, 2020.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...