Na Amri Kilagalila,Njombe
Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mhandisi Marwa Rubirya ameagiza wakuu wa wilaya
na wakurugenzi mkoani humo kusimamia na kufuatilia hatua za kuhakikisha
wasichana wenye umri wa chini ya miaka 14 wanapata dozi mbili na tatu za
HPV ya chanjo ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi.
Akifungua kikao cha kujadili mikakati ya kuinua kiwango cha dozi ya pili
ya saratani ya mlango wa kizazi katika mkoa wa Njombe mpango
unaoratibiwa na Shirika la Jhpiego, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe,
Mhandisi Marwa Rubirya amesema amebaini kuna makundi matatu ya vijana
wakiwemo walioathirika na maambukizi ya VVU hawajapata chanjo hiyo..
"Vile vile hawa wasichana ambao wana maambukizi ya virusi vya ukimwi nao
ni muhimu wakashirikishwa katika zoezi hili la kupata chanjo,na wao
tumejifunza wanatakiwa kupata chanjo tatu"alisema Rubirya
Aidha Rubirya amesema mkoa unaowajibu wa kujifunza mafanikio yaliyopatikana kutoka mikoa mingine.
"Tumejifunza kutoka kwa wenzetu waringa sasa tuje na mikakati ambayo
itatusaidia kuhakikisha tunaendeleza mafanikio amabyo tutayapata
mwishoni mwa programu hii"alisema tena Marwa
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Bumi Mwamasage pamoja
na mratibu wa Afya ya uzazi na mtoto, Felisia Hyera na Dk. Maryrose
Giattas ambaye ni mratibu wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
kutoka shirika la Jhpiego wamesema ni muhimu kupata chanjo ya HPV ili
kuokoa maisha ya wasichana na wanawake hivi sasa..
"Chanjo hii inalenga kuzuia saratani kwa kundi hilo kwani kina mama ndio
wanao patwa na shida hiyo wanapofikia umri uliozidi miaka 30 "alisema
Dk. Bumi Mwamasage
Kikao hicho kilichowashirikisha wajumbe kutoka Taasisi za Dini, Jeshi la
Polisi pamoja na uwakilishi wa wanawake michango mbalimbali kuhusu
namna ya kuwezesha kampeni hiyo ilitolewa.
"Jeshi la polisi nalo lina nafasi kubwa kuhakikisha watoto wanakuwa
salama,na katika kuchukua hatua kwa wale wanaowafanya watoto wasiweze
kupata chanjo"alisema alisema Kamanda Hamis Issa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...