*Atoa ushauri kwa Serikali

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MBUNGE wa HANDENI mjini Reuben Kwagilwa (CCM) amesema kuwa, kupanda kwa bei ya saruji kunaathiri sana wananchi wa hali ya chini jambo ambalo ni kinyume na taratibu na maono ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Joseph Magufuli ambayo daima imekua ikimtetea mnyonge katika katika kupata haki zake za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kwagilwa amesema kuwa, kama taifa lazima litengeneze matajiri wakubwa na kuwekeza kwenye uzalishaji wa bidhaa zenye tija ikiwemo mafuta na saruji.

"Kupanda kwa bei ya saruji kunaathiri wananchi wa hali ya chini kwa kiasi kikubwa, leo bei za cement kwa Mkoa wa Bukoba ni elfu 23,000-24,000, Mwanza elfu 21,000-22,000 na Tarime 22,000 hadi 23,000 bei hii si elekezi na inawaathiri wananchi wa chini." Amesema.

Katika kukabiliana na hilo ameishauri Serikali masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na;

"Kwanza napenda kuishauri Serikali kupitia upya mikataba ya viwanda hasa vipya na vikubwa na kuangalia mambo makubwa ikiwemo kiwango cha uzalishaji walichohaidi, kujua gharama ya mfuko wa saruji kwa bei ya kiwandani na hiyo ni pamoja na kuangalia mnyororo wa usambazaji  kuanzia kiwandani hadi hadi kwa mtumiaji wa mwisho." Ameeleza.

Aidha ameishauri kuondolewa kwa mnyororo wa madalali waliopo katikati ya viwanda na watumiaji kwa kuwa ndipo tatizo linapoanzia.

Vilevile ameshauri kupitiwa upya kwa sera za uwekezaji hasa katika masuala ya uongozi kwa kuwa katika viwanda vingi vya nje zinazoshikwa na wazawa ni zile za chini kabisa (vibarua.)

"Sheria za kazi zifuatwe kikamilifu ili kazi zinazowezwa kufanya na watanzania wazifanye na hii itasaidia katika kulinda ajira za watanzania." Amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...