Na Estom Sanga-TASAF

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeanza awamu ya pili ya zoezi la uhakiki wa  Walengwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF mwanzoni mwa mwaka huu jijini Dar es salaam.

Akifungua kikao kazi cha Wawezeshaji wa kitaifa kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo ya TASAF jijini Dar es salaam, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga,Mkurugenzi wa Programu za Jamii Amadeus Kamagenge amesisitiza umuhimu wa kutekelezaji zoezi la uhakiki wa Walengwa kwa umakini mkubwa ili kuondoa uwezekano wa kuwa na walengwa wasiostahili kunufaika na huduma za Mpango.

‘’Uhakiki na uandikishaji sahihi wa Walengwa ndiyo Msingi wa kuwapata Walengwa sahihi wa kuhudumiwa kwenye Mpango’’ amesisitiza Kamagenge.

Amesema licha ya mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za Mpango ,TASAF imeweka uzito mkubwa kwenye zoezi la uhakiki wa Walengwa  ili wanaokidhi vigenzo ndio wanufaike kama ilivyoagizwa na serikali.

Akitoa maelezo ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya zoezi la uhakiki wa Walengwa ,Meneja wa masjala ya Walengwa wa TASAF ,Bi.Phillipine Mmari amesema asilimia 80 ya Walengwa walihakikiwa katika awamu hiyo iliyofanyika kote nchini. Na asilimia 20 watahakikiwa katika zoezi litakalofanyika katika awamu ya pili.

Serikali kupitia TASAF inatekeleza kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambacho kinatarajiwa kuhudumia takribani Kaya milioni MOJA na Laki NNE ili kuwawezesha wananchi wanaoishi katika umaskini uliokithiri kupata fursa ya kukuza kipato na kuboresha  miundombinu katika sekta za elimu,afya na maji.

Mkurugenzi wa Programu za Jamii-TASAF Amadeus Kamagenge(aliyesimama)  akifungua kikao kazi cha Wawezesha wa kitaifa wa zoezi la kuhakiki Walengwa waTASAF ,kulia kwake ni meneja wa Masjali ya walengwa wa TASAF,Bi. Phillipine Mmari na kushoto  ni Mtaalamu wa Mafunzo Bi. Mercy Mandawa.

Baadhi ya Wawezeshaji wa kitaifa wa zoezi la Uhakiki wa Walengwa wa TASAF,wakiwa kwenye ukumbi wa ofisi ndogo  ya TASAF jijini Dar es salaam wakisikiliza hotuba ya ufunguzi  wa kikao kazi hicho iliyotolewa na Mkurugenzi wa Programu za Jamii Amadeus Kamagenge (hayupo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...