Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Wales Karia akiwapokea
wachezaji wa timu ya Taifa ya wasichana wa chini ya umri wa miaka 17
(U-17) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Wachezaji hao wamerejea nchini
wakiwa mabingwa wa michuano Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini
mwa Afrika, (COSAFA) baada ya kuwafunga Zambia kwenye fainali za
mashindano hayo kwa mikwaju ya penati 3-4 kufuatia sare ya 1-1 mchezo
uliofanyika uwanja wa Nelson Mandela Bay, Afrika Kusini.
Mabingwa wa michuano Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa
Afrika (COSAFA) timu ya Taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17
(U-17) wakishangilia ushindi walioupata dhidi ya timu ya Zambia kwa
kuwashinda kwa mikwaju ya penati 3-4 kufuatia sare ya 1-1 mchezo
ulifanyika uwanja wa Nelson Mandela Bay, Afrika Kusini.
Mwenyekiti wa Soka la Wanawake
nchini Bibi Amina Karuma akiwapokea wachezaji wa timu ya Taifa ya
wasichana wa chini ya umri wa miaka 17 (U-17) mara baada ya kuwasili
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
salaam wakitokea Afrika Kusini waliposhiriki michuano Baraza la Vyama
vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika, (COSAFA) na kuibuka mabingwa.
Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) Wales Karia (aliyebeba kombe) akiwa katika picha ya
pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa ya wasichana wa chini ya umri wa
miaka 17 (U-17) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea Afrika Kusini
waliposhiriki michuano Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa
Afrika, (COSAFA) na kuibuka mabingwa.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Addo Komba (aliyebeba kombe) akiwa katika
picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa ya wasichana wa chini ya
umri wa miaka 17 (U-17) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea
Afrika Kusini waliposhiriki michuano Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu
Kusini mwa Afrika, (COSAFA) na kuibuka mabingwa.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...