Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo (kulia) na Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania Plc Rosalynn Mworia wakikata utepe kuzindua duka la kwanza la kampuni hiyo lililopo mjini Kisarawe, duka hilo litatoa huduma zote kwa wateja wa Vodacom.
Mheshimiwa Jokate Mwegelo akicheza ngoma ya asili kushrehekea kuzinduliwa kwa duka hilo jipya
Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishangilia mara baada ya uzinduzi wa duka hilo lililopo jirani na stendi ya Kisarawe
Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Plc kanda ya Pwani akiwakaribisha wageni waalikwa katika uzinduzi wa duka hilo.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akimkabidhi zawadi ya simu mteja wa muda mrefu wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc Saleh Semjaila, sanjari na uzinduzi wa duka la kwanza la kampuni hiyo lililopo mjini Kisarawe, katikati ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Mwanana Shabani.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...