Mchezaji Mwamvua Seif akishangilia baada ya kupachika mpira kimyani na kufunga bao la nne.

Na Agness Francis, Michuzi Tv
KIKOSI cha timu ya wasichana U-17 ya Tanzania wametoka kifua mbele kwa kuwagaragaza timu ya Comoros mabao 5-1 katika dimba la uwanja wa Oval Stadium nchini Afrika Kusini mchezo uliocezwa leo.
Ambapo katika kipindi cha kwanza timu ya Tanzania imeanza kupata goli la kuongoza dakika ya 20 kupitia kwa mchezaji wake Aisha Masaka, Comoros nao hawakuwa nyuma dakika ya 26 ya mchezo huo wamesawazisha goli hilo kupitia kwa mchezaji wao Noussrat Mistoihi na magori hayo yamedumu mpaka wachezaji wanakwenda mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya wasichana ya Tanzania kushambulia kwa kasi na dakika ya 59 Aisha Masaka tena amepachika goli la pili kimyani.Huku dakika ya 61 Joyce Fred amecheka na nyavu za Comoros na kuifungua timu yake bao la tatu,
Mwanvua Seif dakika ya 82 nae amefanikiwa kongeza bao la nne na goli la tano limefungwa na Ptrotacia Mburda dakika 88 za lala salama.
Ikiwa ni mbio za kuusaka ubingwa wa kombe la Mashindano ya COSAFA kwa wasichana U-17 yalioanza kutimua vumbi jana novemba 3 mwaka huu ambapo wameshikishwa timu kumi kutoka nchi mbali mbali barani Afrika.
Ambazo ni kundi A, Afrika kusini, Eswatini, Comoros, Angola, kundi B, Zambia , Malawi, Lesotho, Huku kundi C zikiwa ni Tanzania , Zimbabwe pamoja na Botswana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...