Wafanyakazi wapya 68 wameajiriwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika ngazi mbalimbali sambamba na kupatiwa mafunzo ya maadili ya utumishi wa umma na kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Katika mafunzo hayo, wafanyakazi hao wametakiwa kuazingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi na kutojihusisha na masuala ya rushwa ambayo inachelewesha na kuzuia utoaji bora wa huduma za afya.
Mkuu wa Idara ya Ajira na Mafunzo wa Muhimbili, Bw. Abdallah Kiwanga amesema hospitali imeajiri wataalamu wa macho, wataalamu wa tiba ya viungo, wahudumu wa afya, wauguzi, wauguzi wasaidizi, watunza kumbukumbu na wataalamu wa maabara.
Afisa Takukuru Kanda ya Ilala jijini Dar es Salaam, Bi. Marcela Sallu akitoa mada kwa waajiriwa wapya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuhusu kanuni, sheria taratibu za utumishi wa umma. Baadhi ya watumishi wa MNH walishiriki pia semina hiyo.
Waajiriwa wapya wakiwa kwenye semina hiyo.
Mmoja wa waajirwa wapya akisikiliza kanuni, sheria taratibu za utumishi wa umma.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...