Na Piason Kayanda, Michuzi Tv 

 

Ligi ya Vodacom premier League imeendelea leo na kushuhudiwa Azam Fc wakishindwa kutamba tena mbele wapinzani wao Ruvu Shooting baada ya kutoa sare ya goli mbili kwa mbili. 

 

Azam fc walianza kupata bao lao la kwanza lililofungwa na Ayoub Lyanga kunako dakika ya 34 ya mchezo na kuenda mapumziko wakiwa wanangoza kwa goli moja.

 

Lakini kipindi cha pili Ruvu Shooting walikuja kwa kasi ya ajabu na kunako dakika ya 53 Emmanuel Martin aliweza kuisawazishia Ruvu shooting ,lakini iliwachukua tu dakika 7 Azam Fc kuweza kuandika goli la pili liliofungwa na Mudathir Yahya kunako dakika ya 60 ya mchezo. 

 

Lakini dakika kumi baadae Ruvu shooting walirudi mchezoni na kunako dakika ya 70 Fully Zullu Maganga Jezi namba 10 mgongoni aliweza kuisawazishia Ruvu shooting kwa goli safi. 

 

Kwa matokeo haya yanawafanya Azam Fc kucheza michezo sita bila matokeo kwenye ligi kuu na inawafanya kufikisha alama 29 baada ya michezo kumi na sita na anakuwa na alama 8 dhidi ya Yanga anaye ongoza ligi kwa alama 37, na Ruvu Shooting anafikisha alama 25 baada ya sare ya leo dhidi ya Azam fc.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...