Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya BabaWatoto Mgunga Mwa Mnyenyelwa akizungumza na watendaji wa MGen Tanzania Insurance ambao pia ni washiriki wa biashara ya taasisi hiyo, wakati walipotembelea Makao Makuu ya taasisi hiyo, pia walipata fursa ya kutembelea vituo na kukutana na baadhi ya watoto hapo jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Baba Watoto Mgunga Mwa Mnyenyelwa akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa MGen Tanzania Insurance ambao pia ni washiriki wa biashara ya taasisi hiyo wakati walipotembelea Makao Makuu ya taasisi hiyo, hapo jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Masoko wa MGen Tanzania Insurance Jackson Kindikwili (kulia,) akimkabidhi hundi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Baba Watoto Mgunga Mwa Mnyenyelwa (kushoto,) ikiwa ni sehemu ya kuchangia kituo hicho kinachowalea watoto waishio katika mazingira magumu, hapo jana jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa MGen Tanzania Insurance wakiwa na watoto wanaolelewa na taasisi ya Baba Watoto kituo cha Mburahati na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hao, hapo Jana jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa MGen Tanzania Insurance wakiwa na watoto wanaolelewa na taasisi ya Baba Watoto kituo cha Ilala na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hao leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...