Baraza la Usuluhishi na Uamuzi(CMA) imehairisha kutoa uamuzi mdogo wa mgogoro wa waliokua wafanyakazi wa Kampuni ya kuzoa taka Jiji la Dar as Salaam, GreenWaste Pro Limited dhidi ya mwajiri wao.

Kutokana na hali hiyo, uamuzi huo utatolewa Desemba 21 Mwaka huu baada ya kukamilika kuandikwa kwa hukumu.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya wafanyakazi hao na mwakilishi wa kampuni hiyo, Msuluhishi wa mgogork huo, Mpulla alidai alidai kuwa, kutokana na mwingiliano wa majukumu, uamuzi huo utatolewa Desemba 21 mwaka huu.

Wafanyakazi hao walikimbilia katika baraza hilo kwa madai ya kuachishwa kazi kinyume na taratibu za kisheria na mikataba yao ya kazi hali iliyosababisha kuishi katika mazingira magumu.

Shauri la wafanyakazi hao lilisikilizwa leo katika Baraza hilo chini ya msuluhishi Mpulla ambapo wafanyakazi 13 waliokua wakifanya kazi katika kampuni hiyo wamedai kuwa, kampuni iliwaondoa kazini bila ya kufuata utaratibu wa kisheria.

Walidai kuwa Februari 12,2020 kampuni hiyo iliwakamata wafanyakazi hao ambao ni 13, na kuwapeleka polisi kwa madai ya wizi wa fedha za kampuni huku akisitisha mikataba ya ajira bila ya kufuata utaratibu wa kisheria.

Walidài kuwa wakati wanakamatwa alikua hawajapewa taarifa yoyote ya kuonyeshs wameachishwa kazi.

Walidai katika kipindi hicho, yeye na wenzake waliwekwa mahabusu kwa siku kadhaa na kwa sababu alikua mjamzito wazazi wake walilazimika kumtafutia dhamana ili waweze kumtoa kwa kuwa siku za kujifungua zilikaribia.

Walidai Kuwa upelelezi wa shauri hilo ulichelewa hali iliyosababisha kushindwa kuwasilisha shauri hilo kwenye baraza hilo kwa wakati.

Aliiomba baraza hilo kusikiliza madai yao na kuyatolea uamuzi ili haki itendeke kutokana na kutolipwa haki zao katika kipindi chote walichokua wanafanyakazi.

Hata hivyo, Wakili wa Kampuni ya GreenWaste Pro Limited, Evans Ignas alidai kuwa hoja zilizowasilishwa na wafanyakazi hao ni batili kwa madai kuwa wanaweza kufungua shauri kwenye barazs hilo hata kama upelelezi unaendelea.

Alidai kuwa, wafanyakazi hao waliondewa kazini kwa kufuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna aliyeondolewa kinyume na kuliomba baraza hilo kutupilia mbali madai hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...