Kamishna
wa Mamlaka ya Bima (TIRA), Dkt. Mussa Juma (kushoto) na Afisa Biashara
Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts wakizindua rasmi huduma ya bima
ambatanishi ya Benki ya CRDB “KAVA Assurance” ambayo inawawezesha
wateja wa ndani na nje ya nchi (diaspora) kupata mkono wa pole wa kati
ya Sh milioni 2 hadi 15 wa matatizo ya msiba au ajali, uliofanyika leo
kwenye ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
====== ====== ======
Kamishna wa Mamlaka ya Bima (TIRA), Dkt. Mussa Juma ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma ya bima ambatanishi ya maisha ijulikanayo kama “KAVA Assurance” kwa wateja wenye akaunti katika benki hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya bima ya Sanlam Tanzania.
Akizungumza
katika hafla hiyo Dkt. Mussa alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo ya bima
kwa akaunti za wateja kutaongeza chachu ya matumizi ya huduma za
kifedha pamoja na kuongeza uelewa wa huduma za bima kwa Watanzania.
“Huduma
hii ya Bima Ambatanishi katika akaunti za wateja imekuja wakati muafaka
ambapo Mamlaka ya Bima imejikita katika kuhakikisha Watanzania wote
wanafikiwa na huduma za kifedha ikiwamo huduma za bima,” alisema Dkt.
Mussa huku akiitaka Benki ya CRDB na Sanlam kujikita katika kutoa elimu
kwa wateja ili kuongeza uelewa zaidi.
Akielezea
kuhusiana na huduma hiyo KAVA Assurance Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na
Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema kupitia huduma hiyo wateja
zaidi ya milioni 3 wenye akaunti Benki ya CRDB watakuwa wakipata malipo
ya gharama za mazishi pindi mteja anapofariki, gharama za usafirishaji
mwili pindi mteja anapofariki nje ya nchi na mkono wa pole pale mteja
anapopata ajali inayopelekea ulemavu wa maisha.
“Endapo
mteja atapa changamoto hizi basi Benki itatoa mkono wa pole kwa ndugu
ambapo kwa wateja wa kawaida mteja atapewa kiasi cha shilingi milioni 2,
wateja maalum wao ni shilingi milioni 5 na shilingi milioni 15 kwa
wanaoishi nje ya nchi (diaspora),” alisema Raballa huku akibainisha kuwa
huduma hiyo ni ya kumuongezea mteja Thamani na hakutakuwa na gharama za
aina yoyote kwa wateja.
Kwa mujibu wa Raballa akaunti zote za Benki
ya CRDB zitanufaika na huduma hiyo ya KAVA Assurance kuanzia Akaunti ya
Akiba, Akaunti ya Watoto “Junior Jumbo”, Akaunti ya Wanafunzi “Scholar”,
Akaunti ya Wanawake “Malkia”, Akaunti ya Diaspora “Tanzanite”, Akaunti
ya Mshahara, Akaunti ya Hundi, Akaunti ya Wakulima “FahariKilimo”,
pamoja na akaunti nyengine.
“Kinachotakiwa
ni mteja kutumia akaunti yake mara kwa mara kwa maana ya kuweka akiba
na kuitumia kufanya miamala mingine ikiwamo ya malipo ya manunuzi ya
bidhaa na huduma kupitia huduma za kidijitali kama CRDB Wakala,
SimBanking na Internet Banking,” aliongezea Raballa.
Akielezea
utayari wa Benki ya CRDB katika kusaidia kusogeza huduma za bima kwa
wateja, Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Bima ya CRDB Bank Insurance,
Wilson Mnzava alisema pamoja na kuanzisha kwa huduma ya KAVA Assurance,
Benki ya CRDB pia ipo mbioni kuingiza huduma ya bima kidijitali ambayo
itawawezesha wateja kupata huduma kupitia simu za mkononi na hivyo
kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
“Nitoe rai kwa Watanzania wengi zaidi kuchangamkia fursa hii kwa kufungua akaunti katika Benki yao ya CRDB, kwa kufanya hivyo tutawezsha kufikia lengo la Serikali la kufikisha huduma za Bima kwa asilimia 50 ya Watazania,” alisisitiza Magabe.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...