Na Amiri Kilagalila, Njombe

JESHI la polisi mkoa wa Njombe linamshikilia mfanyabiashara wa vyuma
chakavu eneo la mizani mjini Makambako aliyefahamika kwa majina ya
Anania Msemwa kwa kukutwa na vyuma vya reli ya TAZARA na vingine
vinavyodaiwa kuibwa kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya
Moronga-Makete.

Kamanda Hamis Issa amebainisha baadhi ya miundombinu iliyokamatwa kuwa ni
pamoja na vyuma vya reli ya Tazara pamoja na vyuma ambavyo vimeibwa
katika miradi ya ujenzi wa barabara ya Moronga -Makete ndani mkoa wa
Njombe.

“Kilichopatikana hapa Makambako ni vyuma vya Reli ya Tazara kwa hiyo
amekamatwa mtu ambaye alikuwa ameviweka nyumbani kwake na huyu mtu ana kibali cha kufanya biashara ya kununua vyuma chakavu na vyuma hivi
vimeshatambuliwa vinatokana na reli na reli inayopatokana hapa ni ya
Tazara”alisema kamanda Issa

Pamoja  na hayo Jeshi la polisi linamshikilia Anania Msemwa mwenye
umri wa miaka 50 mfanyabiashara na mkazi wa Njombe ambaye anajihusisha
na ununuzi wa vyuma chakavu baada ya kukutwa na vyuma hivyo.

“Na tumeweza kukamata vyuma vingine 17 vizito kweli kweli aliyekamtwa
navyo anaitwa Anania Msemwa.huyu ni mfanyabiashara ananua vvyuma
chakavu eneo la mizani Makambako,na vyuma hivi vimetoka kwenye Krushia
ya kupasua kokoto kwenye mradi wa kutengeneza bara bara inayotoka
Moronga-Makete.” aliongeza kamanda Issa.

Kamanda Issa amewataka wakazi wa Njombe kuheshimu miradi ya serikali
inayotekelezwa katika mkoa huo kwa kutoa taarifa na kuwafichua watu
wote wanaojihusisha na kuhujumu miradi hiyo kwa kuiba mafuta , saruji
na baadhi ya vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa miradi hiyo.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...