MBUNGE wa Makete Ndg Festo Sanga amekabidhi na kuzifunga Solar panel tatu ambazo aliahidi atawapatia wananchi wa Kijiji cha Ilindiwe kata ya Mang'oto endapo watamchagua alipopita kuomba kura wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu 2020.

Akikabidhi Solar hizo, Mbunge Festo Sanga amesema;

 "Nilipokuja kuomba kura mliniambia hitaji lenu la kwanza ni Umeme wa Solar kwenye zahanati yenu hii, mlihitaji umeme kwasababu huduma nyingi zinakwama nyakati za usiku na hata zile zinazohitaji umeme. Zahanati hii inategemewa na sehemu kubwa ya wananchi wa Mang'oto, nimeona ni vyema nikaitekeleza mapema ili Mama zetu wanapohitaji huduma ya uzazi waipate masaa yote pakiwa na umeme, Lakini wahudumu wetu wapumzike kutumia tochi kuhudumia wananchi nyakati za usiku. Nawaomba mzitunze solar hizi ili zitusaidie kwa muda mrefu wakati tunahangaikia umeme wa REA". Amesema.

Baadhi ya Wananchi walioshuhudia utekelezaji wa ahadi hiyo wamesema, wameshangazwa na namna Mbunge alivyotekeleza ahadi hiyo kwa uharaka kwasababu ni ahadi ambayo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kwanza wa Mkoa wa Njombe na baadae viongozi wengine lakini haikutekelezeka, 

''huyu Sanga ametupa matumaini makubwa sanaaa sisi wananchi wa ilindiwe tunamuombea kwa Mungu ambariki kwa pale alipotoa kwaajili yetu.'' Amesema mmoja ya wananchi wa Ilindiwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...