SHIRIKA la Utafiti wa Viwanda na Maendeleo Tanzania (TIRDO) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 5 ya mwaka 1979, na kuanzisha maabara ili kusaidia sekta ya viwanda ya Tanzania kwa kutoa utaalamu wa kiufundi na huduma za kuboresha msingi wa teknolojia pamoja na utafiti kwenye viwanda. 

Katika kutekeleza majukumu yake, TIRDO imekuwa ikikabiliana na changamoto ya upungufu wa vifaa vya maabara vinavyotumiwa na watafiti-wanafunzi pamoja na wajasiriamali wanaosindika na kusafirisha mazao ya chakula ndani na nje ya nchi hivyo kushindwa kuthibitisha ubora wa mazao na bidhaa zitokanazo na kilimo. 

Ili kukabiliana na changamoto zinazoyakabili makundi hayo mawili muhimu, TIRDO iliomba na kupatiwa ruzuku ya kiasi cha shilingi Milioni 400 kutoka Serikalini kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Ruzuku hiyo imesaidia ununuzi wa vifaa muhimu vya kuwezesha upimaji wa sumu kuvu, kiwango cha madini katika chakula, kiwango cha viini lishe na n.k. 

Maboresho ya miundombinu ya maabara hiyo yamewezesha kuanza kufanya kazi kwa kupima sampuli mbalimbali za mazao yatokanayo na kilimo kwa kuwanufaisha Watanzania na wataalamu wa TIRDO ambao wameongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao. 

Kwa mujibu wa mtafiti kiongozi wa mradi huo, Dkt. Purificator, mpaka sasa kuna jumla ya wanafunzi-watafiti 47 ambao ni wanufaika katika mazao ya kilimo. Pia kuna wajasiriamali, akiwemo Grace Laizer, mwenye kiwanda kinachotengeneza siagi ya karanga (Peanut Butter) ambaye amekuwa akipima sampuli za karanga anazozizalisha katika maabara hiyo. 

Maabara hii ina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa kwa kuwa imeimarisha udhibiti ubora wa vyakula kwa viwango vya kitaifa na kimataifa. 

 Mkurugenzi wa mradi Dkt Purificator Kiwango akieleza namna mradi unavyotekelezwa.

Mjasiriamali Grace Laizer anayepata huduma ya kuhakiki ubora wa karanga kabla ya kutengeneza siagi.

Mtafiti akionesha namna wanavyopima sampuli  mbalimbali katika maabara hiyo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...