Uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki ni changamoto kubwa duniani ambayo huchangia uharibifu mkubwa wa miundom
binu na afya katika nchi nyingi za
Afrika Pamoja na Tanzania. 
 
Ikiwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza kupanua wigo wa zuio la matumizi ya vifungashio vya plastiki, ambavyo havijathibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Nipe Fagio inaunga mkono uamuzi huo wa serikali na inamatumaini makubwa kuwa Tanzania itafanikiwa katika mapambano dhidi ya plastiki zisizorejeshwa.

Nipe Fagio, taasisi isiyo ya kiserikali inayofanyakazi na jamii, sekta binafsi, na serikali ili kufikia maendeleo endelevu katika sekta ya uongozi wa taka, ni taasisi ongozi ya Zaidi ya taasisi 250 nchini, na mwanachama wa Break Free From Plastic, Global Alliance for Incinerator Alternatives (GAIA), pamoja na kampeni ya Let’s Do It Tanzania inayoongoza Siku ya Usafi Duniani. Nipe Fagio pia ni mwandaaji wa kampeni inayoendelea ya Plastiki Yako Mazingira Yetu na itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali dhidi ya zuio la matumizi ya plastiki zisizorejeshwa nchini.

Akitoa maoni yake juu ya maamuzi hayo ya serikali, Bi Ana Le Rocha, Mkurugenzi Mtendaji wa Nipe Fagio amesema Nipe Fagio ikiwa mstari wa mbele kutafuta suluhisho la tatizo la uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki nchini na mara zote ikikusanya takwimu za taka za plastiki ziletazo matatizo kwa jamii na mazingira, ni lazima tuunge mkono maamuzi ya serikali ya kuzuia matumini ya plastiki, moja kati ya hatua thabiti ya kupunguza madhara makubwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingira unaotokana na plastiki nchini Tanzania.

“Tunafuraha sana juu ya kuongeza wigo wa zuio la vifungashio vya plastiki na tunatumaini kuwa Tanzania itaendelea kuwa katika mstari wa mbele katika kutatua tatizo la uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki na kuongeza zuio zaidi kwenye bidhaa za plastiki zitumikazo kwa mara moja, na hivyo, kuiongoza Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika kuwa ukanda huru wa plastiki zitumikazo mara moja.

“Tunatoa wito kwa asasi za kiraia kuunga mkono zuio hili likiwa kama hatua muhimu katika kuboresha maisha ya jamii, afya na kupunguza uharibifu wa miundombinu unaosababishwa na uchafuzi wa mazingira unaotokana na plastiki,” alisema Bi. Ana.

Katika kuunga jitihada hizo za serikali za kupambana na uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki, Nipe Fagio inahimiza watu binafsi na taasisi kuunga mkono kampeni yake ya “Plastiki Yako Mazingira Yetu” kwa kusaini form kupitia google na/ au kutuma logo zao kupitia linki zifuatazo: 

 http://bit.ly/nfsignplastikiyakomazingirayetu na http://bit.ly/nflogoplastikiyakomazingirayetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...