Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi(CUF)Profesa Ibrahim Lipumba kwa kwa kutumia mamlaka yake ya Kikatiba, amemteua Mbarouk Seif Salim kuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar kuanzia leo Desemba 2, 2020.
Profesa Lipumba kupitia barua yenye kumbukumbu Na. CUF/AK/DSM/MKT/07/2020 ameeleza Mbarouk Seif Salim anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ali Makame Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Novemba 8, mwaka 2020 kutokana na kwenda kinyume na msimamo wa Chama.
Taarifa iliyotolewa leo Desemba 2, 2020, na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF Mhandisi Mohamed Ngulangwa imesema Profesa Lipumba amefanya uteuzi huo leo na kwamba kabla uteuzi huo Mbarouk Seif Salim alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.
"CUF- Chama Cha Wananchi kinampongeza Mheshimiwa Mbarouk Seif Salim kwa uteuzi huu na kinamtakia utekelezaji mwema wa majukumu yake ya Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,"amesema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...