Rais wa Majalisi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof.Ludovic Kazwara kutoka Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya SUA amehaidi kuboresha Bonanza la michezo ya Majalisi kwa mwaka  2021 ili ushiriki uwe mkubwa zaidi.

Ameyasema hayo wakati akifunga Bonanza la michezo ya Majalisi na kutoa zawadi kwa washindi walioshiriki kwenye michezo hiyo iliyofanyika Siku ya Jumatano tarehe 16 Novemba 2020 kwenye viwanja vya michezo vya Edward Moringe Kampasi Kuu SUA.

“Kuna baadhi ya michezo haikuchezwa mwaka huu sababu zilizo nje ya uwezo wetu lakini mwakani tutajiandaa mapema na kuongeza michezo mingi zaidi pia tutahakikisha ushiriki unakuwa mpana zaidi” amesema Prof. Kazwara.

Prof. Kazwara amesema kuwa lengo la michezo ya Majalisi ni kuwakutanisha pamoja Wahitimu na  Wafanyakazi  wa SUA na kuwajenga uhusiano mzuri kupitia michezo mbalimbali kama mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Kikapu, kuvuta Kamba, riadha, kukimbia kwenye magunia, drafti, kurusha tufe na kucheza karata.

Naye Mratibu wa michezo hiyo Dkt. Beda John Mwang’onde ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA amesema kuwa Bonanza la michezo ya Majalisi linafanyikaga mara moja kwa mwaka kwa ajili ya kuwakaribisha tena Chuoni Wahitimu wa SUA katika Chuo hicho.

“Mwaka huu muitikio wa kushiriki kwenye michezo haukuwa mzuri sababu mambo yamekuwa mengi na yameongozana kwa pamoja hasa ukizingatia tupo  mwishoni mwa mwaka watu wengi wameenda kwenye majukumu ya Chuo na ya Kitaifa”  amesema Dkt. Mwango’mbe.

Lakini pia amewapongeza baadhi ya Majalisi na Wafanyakazi wa SUA waliotoa muda wao kwa kushiriki kwenye michezo hiyo kwani michezo ni Afya, michezo ni furaha na michezo ni burudani.

“kwa mwaka huu tumepata washiriki wazuri kama Prof. Elliot Phiri ambaye kwa umri wake tusingetarajia kumuona akikimbia mbio za mita 100  na kushika nafasi ya pili hatukutegemea kabisa hawashinde vijana kwenye mbio hizo” amesema Dkt. Mwango’mbe.

Akitoa neno la Shukrani Makamu wa Rais wa Majalisi Dkt. Raymond J. Salanga ambaye ni Mhadhiri kutoka SUA amewapongeza Majalisi, wafanyakazi na Wanafunzi kwa kujitoa kushiriki kwenye michezo hiyo ya Majalisi pamoja  kuwa na majukumu mengine lakini waliona umuhimu wa kushiriki wenye michezo hiyo.

“Tunakubali kuwa mwaka huu wa 2020 hatukuwa vizuri kama mwaka jana tuombe radhi kwenye mapungufu  yaliyojitokeza ni sababu zilizo nje ya uwezo wetu lakini tunahaidi kujipanga vizuri mwaka 2021” amesema Dkt. Salanga.

SUA Convocation Sports Bonanza ni jumuiko kuu la Alumni wote wa SUA ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka, wiki moja kabla ya kutunuku shahada kwa wahitimu wa shahada za awali hadi uzamivu, maarufu kwa jina la "HOMECOMING WEEK". Ni Jumuiko na sehemu pekee muhimu inayowakutanisha wanazuoni, wafanyakazi na wahitimu wa SUA mwanzoni mwa mwaka wa masomo wakishiriki michezo mbalimbali na kufurahi pamoja. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...