Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

KATIKA kuelekea kwenye Mabadiliko ya Uendeshaji wa Klabu ya Soka ya Yanga, hatimaye Ripoti ya Mabadiliko hayo imekabidhiwa kwa Mshauri wa Klabu, Setho Mbatha ili kuifanyia kazi sambamba na Kamati ya Utendaji, Sekretarieti na Kamati mbalimbali za Klabu hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyeki wa Klabu, Dkt. Mshindo Msolla amesema wanawashukuru GSM katika kufanikisha kikamilifu Ripoti ya Mabadiliko ya Uendeshaji wa Klabu hiyo kwa kushirikiana na La Liga.

Dkt. Msolla amesema lengo la kutaka Mabadiliko hayo ni kuipeleka timu hiyo katika uendeshaji ambapo Wanachama, Wapenzi na Mashabiki watanufaika na uendeshaji huo, amesema watafuata miongozo yote ya Serikali katika uendeshaji huo wa Klabu ya Wananchi.

Dkt. Msolla amesema baada ya kukabidhi Ripoti hiyo, kwa kushirikiana na Kamati ya Mabadiliko itaundwa Kamati itakayoangalia masuala ya Katiba ya Klabu. “Wazo la Mabadiliko ya Uendeshaji wa Klabu liliandikwa katika Katiba ya mwaka 2010, lakini bahati mbaya miaka 10 ilipita bila kuwa na wazo hilo”, amesema Dkt. Mshindo.

“Tutaunda Kamati ambayo itasimamia kurekebisha Katiba ambayo itaendana na masuala yaliyo ndani ya Ripoti ya Mabadiliko ya Uendeshaji wa Klabu, Kamati ya Mabadiliko, Kamati ya Utendaji tutapitia na kujua maeneo ya kipaumbele kwenye Muundo na kupata Wanachama wengi na uwajibikaji wao”, ameeleza Dkt. Mshindo.

Kwa upande wake, Mshauri wa Klabu, Senzo Mbatha amesema wanajivunia kupata ushauri katika Mabadiliko ya Uendeshaji kutoka kwa Washauri wao La Liga na Sevilla kutoka Hispania, amesema Uongozi, Wanachama na Wapenzi wa Klabu watajivunia kuwa na Mfumo bora unaotambulika Duniani.

Pia ameomba ushirikiano wa Wanachama wote klabuni hapo kuhakikisha Mabadiliko ya Uendeshaji wa Klabu yanafanikiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...