Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KAMPUNI ya Riccobs Entertainment imezindua rasmi mradi wa watoto wa kujenga utamaduni wa kujisomea ujulikanao, 'Amani Read To Read' huku balozi wa mradi huo Sasha Mbilinyi akiwashauri watoto kusoma vitabu hivyo vilivyoandikwa kwa lugha rahisi ili kuweza kufahamu mambo mengi yanayohusu Tanzania ikiwemo mbuga za wanyama na rasilimali zake na kuweza kulitangaza Taifa kote ulimwenguni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wakizundua mradi huo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Richard George amesema, mradi huo ni mtiririko wa vitabu vya watoto vinavyolenga kutangaza maliasili na utalii kupitia binti Amani ambaye ni Sasha Mbilinyi.

Amesema katika mtiririko wa vitabu vipatavyo kumi Sasha atakuwa balozi na kubeba sura ya amani na itakua nafasi nzuri kwa watoto kuweza kusoma kujifunza na kuitangaza taifa na kueleza kuwa watafika mashuleni pamoja na kutumia njia nyingine za mauzo ili kuwafikia watoto wengi zaidi.

Vilevile amesema kuwa, vitabu hivyo vyenye picha na vielelezo katika habari vitapatikana kwa lugha saba ikiwemo Kiswahili, Kifaransa na Kireno na asilimia 2 ya mapato ya vitabu hivyo yataelekezwa kwa watu wenye sikoseli.

Kwa upande wake balozi wa mradi huo Sasha Mbilinyi ameeleza kufurahishwa na kuchaguliwa kuwa balozi wa vitabu hivyo na kuahidi kuwa kiongozi bora kwa watoto wengine kwa kuwahimiza kusoma vitabu hivyo vinavyoeleza utalii na maliasili ya Tanzania.

Sasha amesema, atakuwa balozi bora kwa kuhakikisha watoto wanapenda kusoma vitabu zaidi na kujiongezea maarifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...