Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kilichoshirikisha waliokuwa waangalizi wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu,kutoka majimbo sita ya Arusha,wakiwa katika picha ya pamoja na watekelezaji wa mradi wa IDIET,unaotekelezwa na TAWLA, jijini Arusha.
 
Na mwandishi wetu, Arusha.

CHAMA Cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA,) tawi la Arusha, kimekutanisha waliokuwa waangalizi wa Uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu kujadili  na kutoa mrejesho kuhusu uchaguzi huo.

Wadau hao walikutana jana jijini Arusha  walitokea katika majimbo ya Longido, Monduli, Karatu, Arumeru Mashariki na Arumeru Magharibi.

TAWLA ilikutanisha wadau hao kupitia mradi wake wa IDIET ambao wanautekeleza katika mikoa mbalimbali hapa nchini nambao unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).

Akizungumza katika majadilianao hayo yaliyofanyika jana mmoja ya watekelezaji wa mradi huo kutoka TAWLA,Clara Chuwa alisema mradi huo una lengo la kuangalia ushiriki wa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Alisema katika mradi huo wanashirikiana na Taasisi ya Vijana ya TYC na kuwa moja ya kazi walizofanya ni kuangalia ushiriki wa makundi hayo ambapo mradi huo unatekelezwa katika mikoa ya Mwanza,Tanga na Arusha.

Kwa Mkoa waArusha mradi  ulikuwa unatekelezwa katika Wilaya za Arumeru(yenye majimbo mawili),Monduli na Karatu na ulifanywa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile serikali na vyama vya siasa.

“Tunashukuru wadau kwani tumeshirikiana na kusaidia kufanikisha lengo zima la mradi ambalo ni kuangalia ushiriki wa walengwa wa mradi.”alisema Clara.

Naye Elibariki Laizer,ambaye alikuwa  mwangalizi wa uchaguzi jimbo la Monduli,alisema uchaguzi huo ulikwenda vizuri na kuwa baadhi ya maeneo yalikuwa na changamoto ndogo ambazo ziliweza kutatuliwa na uchaguzi kuendelea.

“Kulikuwa na changamoto kidogo ambazo zilitokea katika vituo ila nyingi ni ndogo ikiwemo wasimamizi wa kata kutotaka tukae kwenye vituo ila alipopita Msimamizi wa Jimbo aliwawataka watuache tubaki na kuangalia zoezi zima la ychaguzi mpaka zoezi la kuhesabu kura.” Alieleza.

Mmoja wa washiriki  Biliuda Kisaka,alitaja miongoni mwa changamoto walizobaini kwenye vituo ni pamoja na watu wa makundi maalum ikiwemo walemavu wa viungo kutokuwa na miundombinu rafiki.

“Tunaomba serikali itenegneze mazingira mazuri kwa makundi maalum katika chaguzi zijazo ili kuwawezesha kutekeleza haki zao ya msingi ya kikatiba kwani miundombinu katika vituo vingi haikuwa rafiki hasa kwa maeneo ya pembezoni.

Kwa upande wake mwezeshaji wa majadiliano hayo, Firimini Miku alisema katika kikao kazi hicho wadau hao walijadiliana mafanikio,changamoto na maboresho kwa wadau na sekta binafsi na nini kifanyike ili kuboresha changuzi zijazo.

“Katika majadiliano haya tumeona bado serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wana wajibu wa kuendelea kutoa elimu zaidi ya mpiga kura hasa maeneo ya vijijini.”alisema

Immelezwa kwa upande wa vyama vya siasa bado wanahimizwa kutenda haki na kutoa fursa kwa vijana na wanawake katika kuwania nafasi za uongozi,ili kuongeza idadi yao katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...