
Na Eleuteri
Mangi, WHUSM-Dar es Salaam
USIKU wa Desemba 26, 2020 utakuwa ni mwendelezo wa matamasha ya kufunga mwaka
yanayowahusisha wasanii na wananchi katika kuburudika na kusherehea mafanikio
ya kazi za Sanaa nchini.
Tamasha
la Muziki la Serengeti limekuja kunogesha siku ya kufungua zawadi ambapo linahusisha
wasanii kwa lengo la kuwaletea watanzania furaha, amani, utulivu, utu wema na udugu
ambavyo ni tunu za taifa ambazo na nyenzo za kulisaidia taifa na Watanzania kufikia
maendeleo endelevu.
Siku
hiyo itawafanya watanzania kuwa na siku yenye bashasha kufurahia kazi za
wasanii wetu na kuenzi kazi zao ambazo kila mara zimekuwa kioo cha nchi yetu na
kimataifa. Ufundi wao wa kazi ya sanaa umekuwa msingi adhimu wa kumfanya mtanzania
na wapenzi wa muziki wa Bongo fleva kufikisha fikra au mawazo ambayo yanasaidia
kuelimisha, kuonya, kuburudisha na kufundisha jamii.
Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia sekta
ya Sanaa ipo mstari wa mbele kwa kushirikiana na wadau wengine kuratibu,
kusimamia na kutekeleza tamasha la Serengeti Music and Art Festival ambalo
litakalofanyika Desemba 26, 2020 katika Uwanja wa Uhuru.
Kutokana
na umuhimu wake, wamejitokeza wadau kadhaa ambao wameunga mkono wazo la tamasha
ambalo linalenga kuwaleta pamoja na kuwaunganisha wasanii mbalimbali kupitia
kazi zao za sanaa.
Wadau
hao ni kampuni ya Multichoice, redio EFM, Clouds media, redio 5, Peramiho DJ’s,
Global TV, Elsewedy Electric, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA),
Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN),
Chanel 10, Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Shirika la Mawasiliano la
Tanzania (TTCL), Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam
(DAWASA) pamoja na benki za NMB, CRDB.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali
Dkt. Hassan Abbasi amewathibitishia Watanzania tamasha hilo limekuja muda
mwafaka na ni tamasha la kipekee ambalo litawaleta pamoja wasanii na wananchi.
Uamuzi
wa kufanyika kwa tamasha hilo ni taswira ya uamuzi mahiri alioutangaza Dkt.
Abbasi Desemba 02, 2020 Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na wasanii
wa tasnia ya filamu ambapo alisisitiza kuwa siku hiyo itakuwa ni maalum kwa
ajili ya kusherekea sanaa za Tanzania.
Hakika
huu ni mwanzo mpya katika sekta ya Sanaa kuwa na tamasha ambalo linawaleta
pamoja wasanii wakongwe na chipukizi ili waweze kubadilisha uzoefu hatua ambayo
imekuwa na mwitikio mkubwa wa wasanii ambao wamelipokea kwa furaha na
kuthibitisha ushiriki wao.
Hadi
sasa zaidi ya Wasanii 60 wamethibitisha kushiriki tamasha hilo wakiwemo wasanii
wa muziki wa kizazi Kipya (Bongo Fleva) wa sasa na wazamani, wamuziki wa nyimbo
za Injili, singeli, sanaa za maonesho kama maigizo na sarakasi na pia filamu
fupi za Bongo Movie.
Idadi
hiyo ya wasanii inaleta taswira ya ushirikiano, Amani na upendo miongoni mwao. Wasanii
hao ni pamoja na Sholo Mwamba, Nandy, Mrisho Mpoto, Christina Shusho, Kala
Jeremiah, THT, Aslay, Becka Fleva, Shilole, Chege, Snura, Jesca Mshama, Dogo
Janja, Dulla Makabila, Baby Madaha, Stamina, Meja Kunta, GoodLuck Gozbert,
Linah, Barnaba, Young Dee, Mabantu, Msechu, Pam D, Msami, Madee, Whouz, Fid Q,
Weusi, Maarifa, Rapcha, MoniCentralZone, Baddest 47 and Dully Sykes
Huku
wasanii wanaowakilisha Bongo Fleva wa awali ni Inspector Haroon, Matonya, Z
Anton, Tunda Man, Kassim Mganga, TID, Feruz, Soggy Dogg, Chid Benz, Mb Dog,
Wateule, Wagosi wa Kaya, East Coast Team, TMK wanaume na Mtafya na Nini
Kufanyika
kwa tamasha hilo ni utekelezaji wa sera ya kitaifa ya maendeleo ya Sanaa hatua
inayosaidia kusisitiza matumizi ya maadili ya kitaifa katika shughuli za
muziki, sanaa za maonesho na ubunifu kwa jumla.
Tamasha
hilo litaanza Saa 08:00 Mchana katika Uwanja wa Uhuru mpaka Alfajiri na
kiingilio ni Tsh. Shilingi 5,000 na fedha hizo zinalipwa kwa mfumo wa N-CARD
ambazo zinapatikana katika maeneo mbalimbali ikiwemo Maduka ya Sunderland
Sports Wear-Mtaa wa Kariakoo/Nyamwezi, Merere Sports Wear - Kariakoo Mkabala na
Big Bon Msimbazi, Maduka ya Shafii Dauda-Sinza Makaburini na Tabata, Maduka ya
Vunja Bei-Sinza Madukani, Sinza Makaburini na Kinondoni pamoja na Uwanja wa
Uhuru ambapo kadi hizi zitakuwa zikiuzwa muda wote kabla na siku hiyo ya
tamasha. Lipia tiketi yako sasa kupitia huduma za kifedha za M-Pesa, Tigo Pesa,
Airtel Money pamoja na T-Pesa.
Mapato
na matokeo ya tamasha hilo yanatarajiwa kuwa chachu ya kuendeleza mifumo ya
kutambua wasanii katika kutekeleza shughuli za maendeleo ya sanaa.
Aidha,
Dkt. Abbasi ameongeza kuwa burudani itaendelea Desemba 27, 2020 katika Taasisi
ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ambalo linahusu kazi mbalimbali za
Sanaa ikiwemo uchongaji, uchoraji, burudani za asili za sarakasi na ngoma.
Tamasha hilo halitakuwa na kiingilio ambapo watu wote wanakaribiwa kufurahia
ubunifu na kazi za Sanaa za maonesho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...