Mwenyekiti wa Bodi Ya Wakurugenzi wa TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis R. Semfuko akinunua Nyamapori kihalali kumuunga mkono Mfanyabiashara wa Bucha hiyo ya Nyamapori na baadae kukabidhiwa risiti za mashine ya EFD.

Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis R. Semfuko Leo
tarehe 20/12/2020 Jijini Dodoma amezindua bucha ya kwanza ya nyamapori
nchini kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa mapema mwaka huu.
Hafla
hizo za Uzinduzi zilifanyika maeneo ya chang'ombe Mtaa wa Stendi ya
Zamani Makao Makuu ya Nchi Dodoma, ambapo Mwenyekiti huyo wa Bodi
aliambatana na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Bw. Mabula Misungwi pamoja na
wajumbe wa Bodi hiyo ya TAWA.
Aidha,
bucha hii imekuwa ya kwanza kati ya bucha 46 zilizopata usajili baada
ya Kamati ya Kumshauri Kamishna kuhusu bucha za kuuza nyamapori kuridhia
kufuatia kanuni ya bucha ya mwaka 2020 ambayo iliundwa baada ya Tamko
la Mh.Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli la Mwezi Machi mwaka huu
kutaka kuanzishwa bucha za nyamapori Tanzania.
Wananchi
wa Viunga vya jiji la Dodoma leo walifurika maeneo ya chang'ombe
kushuhudia zoezi hilo la Uzinduzi na kufurahia fursa ya kupata kitoweo
adimu cha Nyamapori, ambapo Mara baada ya zoezi la Uzinduzi wananchi hao
walijaa katika bucha hiyo inayomilikiwa na Mfanyabiashara aitwaye
Bw.Samson Joel Kitangengi na kujinunulia kitoweo hicho.
TAWA
imetekeleza kikamilifu agizo la Rais wetu na hivyo ni imebaki zamu ya
wananchi wa Tanzania kufurahia fursa hadhimu ya rasilimali za
wanyamapori wetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...