***************************
Na Piason Kayanda, Michuzi Tv
Droo ya 16 bora ya mashindano ya klabu bingwa barani ulaya imetangazwa rasmi mara baada ya kumalizika kwa hatua ya makundi wiki iliyopita.
Chelsea chini ya Frank Lampard wanakutana na Atletico Madrid ambao ni vinara wa ligi ya Uhispania Laliga, Liverpool wakiwa na majeraha ya wachezaji wake muhimu wanakutana na RB Leipzig ambao waliwaondoa Manchester united kwa kuwafunga goli tatu kwa mbili.
Manchester City itasafiri kwenda Ujerumani katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo kumenyana na Wajerumani Borussia Monchengladbach,Pep Guardiola naManchester City yake wanatarajiwa kupigana kwa nguvu kuweza kufika nusu fainali na Fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo ambayo inaishiaga robo fainali tu.
Vita ambayo inasubiliwa kwa hamu ni vita ya Neymar dhidi ya mshikaji wake Lionel Messi ambapo Barcelona watakipiga na Paris Saint-Germain amabapo mara ya mwisho timu hizi kukutana Barcelona waliwatoa Paris Saint- Germain kwa kipigo cha goli sita kwa moja.
Mechi nyingine ni Real Madrid watakao wakabili Atalanta,Sevilla atakipiga na Borrusia Dortmund, na Juventus wakutana na Porto ya huko nchini Ureno.
Huku mabigwa watetezi wa mashindano hayo ya klabu bingwa Barani Ulaya 2019/2020 Bayern Munich watachanga karata zao kwa mara nyingine tena kuelekea kutetea ubingwa wao dhidi ya Lazio ya huku nchini Italia
Mzunguko wa 16 unatarajiwa kufanyika Februari na Machi mwaka ujao wa 2021 ambapo tutaenda kushuhudia atae beba ubingwa kwa mwaka 2020/2021.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...