Na Jane Edward,Michuzi TV Arusha
Wananchi wa Wilaya ya Meru Mkoani Arusha wengi wao WAKIWA kutoka familia zisizo na uwezo wa kifedha wamepatiwa huduma ya matibabu ya bure ya magonjwa mbalimbali kutoka kwa madaktari bingwa kutoka hospitali za serikali huku idadi kubwa wakigundulika kusumbuliwa na magonjwa ya macho pamoja na shinikizo la damu hali inayotajwa kusababishwa na mfumo wa maisha wanayoishi
Zoezi hilo limefanyika leo katika kiwanja cha Leganga ikiwa na lengo la kuwafikia Wana Arumeru zaidi ya mia mbili
Matibabu hayo ambayo yameratibiwa na kampuni ya Phide kwa kushirikiana na hospital ya Mkoa ya Mount Meru,ambalo MkurigenI wa kampuni hiyo Phidesia Mwakitalima amesema kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza mara nyingi hayapewi kipaumbele kwa kuwapima wananchiena hivyo wao wameonyesha njia ili kuokoa wananchi walio wengi.
Kwa upande wake mtaalamu wa afya kutoka hospitali ya Mkoa ya Mount Meru Juma Muna amesema kuwa uhitaji wa wananchi kupimwa magonjwa ambayo si ya kuambukizwa ni mkubwa na kwamba kitendo hicho kuonyesha kujali afya za wananchi hasa wenye hali duni.
"Vipimo hivi vya macho,presha,shinikizo la damu ,kisukari,ni miongoni mwa magonjwa yanayosumbua Sana jamii yetu kwakuwa wengine hushindwa kupima kutokana na umbali wa hospitali ama fedha,kwahyo fursa hii itumiwe na wadau wengine kufanya zoezi kama hili ikiwemo na uchangiaji damu"Alisema Juma
Vile vile baadhi ya wananchi waliopatiwa huduma hiyo wamesema upimaji huo imekuja wakati muafaka kwakuwa wengi wao hawana uwezo wa kifedha kugharamia matibabu hayo katika maeneo yao wanayoishi.
Zoezi hilo ni zoezi la nne toka kuanzishwa kwa utaratibu huo wa upimaji na kampuni hiyo ambapo watu takribani mia NNE wameshanufaika na zoezi hilo.
Phidesia Mwakitalima, Muandaaji wa zoezi la upimaji afya katika Wilaya ya Meru akizungumza na vyombo vya habari juu ya zoezi hilo. (Picha na Jane Edward, Michuzi TV Arusha).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...