Na Patricia Kimelemeta

Wazazi wameshauriwa kuwapeleka watoto kliniki ili waweze kupatiwa dawa za Vitamin A na za kutibu maambukizi ya minyoo ambayo uchangia udumavu kwa watoto.

Nayo yalisemwa hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisj ya Chakula na Lishe,Dk. Elifatio Towo kwenye semina ya waandishi wa Habari iliyofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo mwezi huu ni mwezi wa Afya na Lishe ya mtoto.

Dk. Towo amesema kuwa, ili mtoto aweze kukua vizuri anahitaji  kunyonya maziwa ya mama yake kuanzia umri wa siku 0 hadi anapotimiza unri wa miezi sita, baada ya hapo anatakiwa kula vyakula mchanganyiko huku akiendelea kunyonya.

Alisema kuwa, katika kipindi hicho, mtoto anatakiwa kupewa Vitamin A ambayo utoka kila baada ya miezi sita pamoja na dawa jumuishi za kutibu maambukizi ya minyoo ambazo ni muhimu katika ukuaji wake ili kumkinga na magonjwa mbalimbali ambayo yatamrudisha nyuma kwenye ukuaji.

Alisema kutokana na hali hiyo, wazazi au walezi wanashauriwa kuzingatia ushauri nasahaa unaotolewa na watalaam wa afya ili waweze kuwalea watoto wao katika mazingira bora na salama.

" Katika kipindi cha mwezi wa afya na lishe ya mtoto, ambayo ni mwezi aa sita na 12, wazazi na walezi wanashauriwa kuwapeleka watoto wao kliniki ili waweze kupewa huduma jumuishi ikiwamo dawa za kutibu maambukizi ya minyoo, hali hiyo itamsaidia mtoto kuwa na afya bora na kumkinga na magpnjwa,"alisema Dk. Towo.

Aliongeza kuwa, Serikali imekua ikitumia jitihada mbalimbali ili kuhakikisha kuwa,wazazi na walezi wanapata elimu bora ya namna ya kuwalea watoto wao na kuwakinga na maradhi ambayo yanaweza kuwasababishia udumavu katika ukuaji wao.

"Mwaka jana tuliweza kuwafikia watoto 8,674,656  nchi nzima ambayo walipewa huduma jumuishi ikiwamo dawa za minyoo, jambo ambalo limewasaidia kukua katika hali nzuri na kwenye afya bora.

Alisema kuwa,hayo ni matokeo chanya katika kuhakikisha kuwa, elimu ya malezi na makuzi bora inawafikia walengwa wengine na wazazi au walezi kuhamasika kuwapeleka watoto wao kliniki ili waweze kupatiwa huduma jumuishi.

Alisema kuwa, licha ya kuwepk kwa mafanikio hayo, lakini bado kina changamoto kwa baadhi ya watoto ambayo hawajapatiwa huduma jumuishi wamekuwa wakipata marafhi ya mara kwa mara, kukosa kinga mwilini,kuwa na upungufu wa vitamin A na kutoona vizuri.

Alisema kuwa, kutokana na hali hiyo, serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha elimu zaidi inatolewa kwa wazazi na walezi ili waweze kuwa na makuzi bora.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...