Afisa Tarafa Itiso iliyopo Wilaya ya Chamwino Remidius Emmanuel  amegeuka mbogo na kumtaka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwiyendaje iliyopo Kata ya Haneti Frank Kimbindu kujieleza na kutoa sababu zilizopelekea kusuasua kwa ujenzi wa  vyumba viwili vya Madarasa kupitia fedha za mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R ) tangu  fedha hizo zilipotolewa na Serikali Juni 2020 na matumizi yake  kuanza mapema Mwezi Agosti, 2020.

Afisa Tarafa amehoji mbele ya kikao chake  kilichohusisha Serikali ya Kijiji cha Mwiyendaje, Kamati ya Shule, Kamati ya Ujenzi na viongozi wa kata ya Haneti akiwa ziarani shuleni hapo huku akimtaka Mkuu wa Shule hiyo kueleza ni kwa nini licha ya Serikali kutoa fedha zote Milioni 40 lakini hadi leo  bado ujenzi huo uko hatua ya msingi tena ndo wanaendelea  kujaza kifusi kwenye msingi na kumtaka aeleze nani amekwamisha ujenzi huo wakati fedha zipo ?

"Hii haingii akilini kabisa, yaani Serikali imetoa fedha za ujenzi kwa aslilimia 100,  wenzako mfano Shule ya msingi Dabalo ndani ya Tarafa hii  wao walisha kamilisha  ujenzi huu tangu Mwezi Desemba, 2020  nyinyi leo hata jamvi bado? Sasa nahitaji uandike maelezo ya kina unifahamishe na kujieleza  sababu zipi ambazo zimetufikisha hapa na ueleze nani anatakiwa kuwajibika katika hili" Remidius Afisa Tarafa Itiso.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu huyo amesema kilichopelekea kusuasua  kwa mradi huo ni kutokana na taratibu za mfumo wa kifedha  pamoja na  kupanda kwa bei ya Saruji bei iliyotofautiana na mchanganuo wa gharama za  ujenzi (BOQ) na hivyo  kusubiri bei ishuke, hata hivyo maelezo hayo yamepingwa vikali na Afisa Tarafa huku Mwalimu huyo akishindwa kujibu pale alipoulizwa Je ujenzi wa sasa unaendelea baada ya bei ya Saruji kushuka ? na wale ambao tayari wamekamilisha  chini ya mradi huu, wao bei haikupanda ? Nakumbuka bei ilipanda Novemba,2020 sasa sababu hizi hazina mashiko katika hili" Amesema Remidius.

Afisa Tarafa ndani ya kikao hicho amelazimika kumpigia simu moja kwa moja Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambaye amefafanua na kuelezea  "kufikia mwezi Agosti, 2020  mifumo wa fedha ilikuwa imefunguka tayari kwa matumizi sahihi ya fedha hizo" tofauti na madai ya Mwalimu mkuu huyo wa Shule amejaribu kujificha katika kivuli cha mfumo wa fedha.

Kijiji hiki mnayo bahati ya pekee, ni Kijiji cha Mwiyendaje ambacho Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli Tarehe 26 Oktoba,2020 akiwa hapa Haneti amehadi kutatua changamoto ya Zahanati, Umeme, kuwajengea Daraja kubwa (Mwiyendaje - Kwahemu), Bwawa  kwa ajili ya shughuli za  kilimo na barabara hii ya Haneti - Zajilwa, sasa kama mnasusua katika miradi hii maana yake mnatia shaka kwa miradi mingine na kufanya kata na tarafa kutiliwa shaka" Remidius.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo amewataka  Mtendaji wa Kijiji na Kata pamoja na Afisa Elimu  Kata hiyo na wao kueleza kwa maandishi kwa nini wameshindwa kusimamia kikamilifu mradi huo kupitia nafasi zao na  kwamba walipaswa kufanya ufuatiliaji wa  hatua zote za  Mradi huo.

Mapema kabla ya kuwasili Mwiyendaje Afisa Tarafa amefanya ziara katika Shule ya Sekondari Haneti kwa lengo la  kukagua na  kupokea taarifa ya ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa pamoja na kufanya kikao cha ndani na kamati ya Ujenzi  na kisha  kupokea taarifa ya kuwasili kwa Wanafunzi shuleni hapo tangu kufunguliwa rasmi kwa shule zote nchini tarehe 11.01.2021.

Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel  akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Shule na  Serikali ya Kijiji cha Mwiyendaje baada ya kutofurahishwa  na kusuasua kwa mradi wa EP4R  (Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa)  vilivyokuwa vimetengewa Shilingi Milioni 40 ambazo tayari zilitolewa na Serikali na kuanza matumizi tangu Agosti, 2020.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa hadi tarehe 12 Januari, 2021 toka Afisa Tarafa Remidius Emmanuel alipofanya ziara shuleni hapo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...