Na Mwandishi wetu, Manyara
ALIYEKUWA
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa chama cha ushirika cha Rift Valley
Cooperative Union (RIVACU) Lohay Langay anashikiliwa na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kwa kutoa ajira bila idhini ya
bodi ya wakurugenzi wa chama hicho.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mjini Babati, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara,
Holle Joseph Makungu amesema Langay anatuhumiwa kufanya kosa hilo
Novemba mosi mwaka 2017 akiwa Mwenyekiti wa RIVACU.
Makungu
amesema Langay akiwa Mwenyekiti wa RIVACU alitumia vibaya nafasi yake
kwa kuingia mkataba wa ajira ya uhasibu kwa Paul Makoye bila idhini ya
bodi ya wakurugenzi wa chama hicho cha ushirika.
"Katika
uchunguzi wetu tumebaini kuwa katika mkataba huo Makoye aliingia
mkataba bila idhini ya bodi ya wakurugenzi wa chama hicho cha ushirika
na kujipatia ujira usio wa haki wa shilingi milioni 2.6," amesema
Makungu.
Amesema kitendo
cha kuajiri bila kibali ni kosa la matumizi mabaya ya ofisi kinyume na
kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya
mwaka 2007.
"Langay anatarajiwa kufikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa Manyara na kusomewa shtaka hilo na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Wakili Martin Makani," amesema Makungu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari Mjini Babati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...