Mabondia wa Tanzania watapata fursa kubwa ya kupromoti vipaji vyao kimataifa kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa ushirikiano baina ya kampuni ya Jackson Group na kampuni ya kimataifa inayo shughulika na masuala ya ngumi za kulipwa ya Global Boxing Stars (GBS).

Moja ya fursa hizo ni kuonekanna nchi nyingi duniani  kupitia ushirikiano wa makampuni hayo mawili ambapo mapambano yao yataonyesha na washirika wengine wa GBS.

Mabondia wa kwanza kufaidika na fursa hiyo ni pamoja na Ibrahim Class ambaye atazichapa na Dennis Mwale kwenye pambano la ubingwa wa mabara wa WBF lililopangwa kufanyika Januari 29 kwenye ukumbi wa Next Door Arena katika usiku uliopewa jina la GBS and Jackson Group Fight Night. Usiku huo pia utakuwa na mapambano mengine saba mbali ya ya lile la Class.

Mbali ya pambano hilo, pia kutakuwa na mapambano mwengine sita tofauti ambayo yatafanywa na Jackson Group na GBS. Mapambano hayo yatafanyika nchini kwa mujibu wa Mkurugenzi wa GBS, Jeremy Bean.

Alisema kuwa mbali ya mapambano hayo, pia mabondia wa Tanzania watapata fursa ya kushiriki katika mapambano makubwa wa ngumi za kulipwa  duniani.

Kwa uoande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Jackson Group, Kelvin Twissa alisema  kuwa wamedhamiria kuleta maendeleo makubwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.

Twissa alisema kuwa aliposema kuwa lengo lao ni kubadili muonekano wa mchezo wa ngumi za kulipwa hakuwa anatania na ushirikiano wao wa GBS ni mwanzo wa muelekeo mpya wa ngumi za kulipwa.

“Tumedhamiria kuleta maendeleo makubwa na ndiyo maana sasa tumeingia makubaliano a GBS, kuna mambo mengi mazuri yanakuja katika ngumi za kulipwa na naamini tutafikia lengo letu,” alisema Twissa.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...