Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Kazi Maduhu akizungumza wakati akizindua ugawaji wa hati za viwanja na mashamba zilizotolewa na kampuni ya Cholemu Investiment inayojishughulisha na miradi ya kupima viwanja na mashamba na kuuza bei nafuu ambapo amewataka kuendelea kufuata sheria na kuwa waadilifu zaidi, Leo  jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Cholemu Investiment Peter Mayunga, Kampuni  inayojishughulisha na miradi ya kupima viwanja na mashamba na kuuza kwa bei nafuu akizungumza na wateja mbalimbali waliokabidhiwa hati zao  na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi leo, jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Kazi Maduhu (Kushoto)akikabidhi hati ya kiwanja kwa mteja Rahma Ahmed mkazi wa Temeke ambaye ni mteja wa kampuni hiyo kulia ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Cholemu Investiment, Peter Mayunga. Leo jijini Dar es Salaam.

Vijana na wateja mbalimbali wa kampuni hiyo waliohudhuria katika shughuli hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KAMPUNI ya uuzaji wa viwanja na mashamba kwa mkopo usio na riba wala dhamana ya Cholemu Investment Limited imepongezwa kwa juhudi inayoonyesha  katika utoaji wa elimu na kuuza viwanja na mashamba kwa kuzingatia sheria za ardhi na mipango Miji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa semina kwa vijana pamoja na kutoa hati kwa wateja waliofanikiwa kumiliki ardhi kupitia kampuni hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Kazi Maduhu amesema, taarifa za upimaji, upangaji na uuzaji wa ardhi ni muhimu kwa wananchi ili waweze kufanya machaguo sahihi na kuepukana na migogoro ya ardhi.

"Kinachofanywa na Cholemu ni cha kuigwa hasa kwa kutoa taarifa sahihi za ardhi, Ukimiliki ardhi wewe sio maskini... sisi kama Manispaa tutahakikisha wananchi wanafikiwa na taarifa sahihi za ardhi pamoja na kutambua haki zao hasa za umiliki wa hati." Amesema

Amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakinunua ardhi na kupuuza suala la umiliki wa hati.

"Manispaa ya Kinondoni tuna hati 735 hazijachukuliwa na hii inadhihirisha kuwa watu hawa hawalipi kodi jambo linaloweza kuwapoteza umiliki wa ardhi, wananchi watambue kuwa hii ni haki ya kila mmliki wa ardhi na anachotakiwa ni kuipata, kuitunza na kulipa kodi." Amesema.

Pia amewapongeza Cholemu Investment Limited kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kupanga, kupima ardhi na kutoa taarifa sahihi kuhusiana na upatikanaji wa ardhi na kuwataka  kukutana na kata kumi za Manispaa hiyo na kutoa elimu zaidi pamoja na kuendelea kufuata sheria, taratibu na kuwa waadilifu.

Kwa upande Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Peter Mayunga amesema, wamekuwa wakiuza ardhi kwa wazawa kwa mkopo usio na riba na dhamana pamoja na kutoa hati kwa wateja wao.

"Tumekuwa tukishirikiana na wataalamu wa  Manispaa katika upangaji wa Miji kwa kuhakikisha wananchi wanapata ardhi isiyo na migogoro.

Ameeleza kuwa malipo ya viwanja hufanyika kidogo kidogo na kwa awamu na wanapatikana katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Pwani na Dodoma.

Vilevile amesema kuwa, vijana ni nguzo muhimu katika kulipeleleka taifa mbele zaidi kwa kuwekeza katika ardhi.

"Tunaendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwapa elimu zaidi hasa ya umuhimu wa kumiliki ardhi na hati....hii ni moja ya changamoto tunayokumbana nayo tuna hati 80 za mashamba ambazo hazijachukuliwa hadi sasa " amesema.

Semina elekezi hiyo iliyowakutanisha na vijana imekwenda sambamba na utoaji wa hati za umiliki wa ardhi kwa wateja waliohudumiwa na kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...