Diwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto akimkabidhi daftari na Kalam mzazi na mlezi  Tabu Adam wakati utoaji Msaada kwa ajili ya wanafunzi wenye changamoto ya kiuchumi katika familia.
Mlezi wa Mwanafunzi  Fatuma Kaloli akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana msaada alioutoa Diwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto.
Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Shule ya Sekondari Mzimuni Seleman Kombo akizungumza kuhusiana na msaada wa daftari na kalam uliotolewa na Diwani.
Diwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto (Kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na uratibu wa utoaji wa msaada Vifaa vya wanafunzi wa Kata hiyo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani Abdallah Kitumbi (Kulia) akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wenzake kuhusiana kujitoa Diwani kwa wananchi wake.
 


*Aahidi kuanzisha Diwani Fund ya kukopesha wananchi wake bila riba

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

WANAFUNZI wenye changamoto za kiuchumi za kifamilia  zinazosababisha kushindwa kusoma kwa kukosa Vifaa mbalimbali katika kata ya Mzimuni zimeweza kutatuliwa na Diwani wa Kata hiyo.

Diwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto alifanya jitihada za kutoa daftari na Kalam ambapo kumeibuka uwepo wa wahitaji wengi kuliko alivyofikiri.

Vifaa hivyo zimenufaika shule ya za Msingi na Sekondari katika kata hiyo  na  zaidi ya wanafunzi  50.

 Manfred Lyoto ni wa Diwani wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo vifaa hivyo ilikuwa ni sehemu ya kushughulikia changamoto ya elimu.

Wanufaika wa msaada huo hasa walezi wa watoto hao walisema kuwa wanampongeza Diwani huyo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia watoto wao kwani uhitaji wa vifaa hivyo ulikuwa ni mkubwa na kwamba wakati watoto wao au majukumu walitaka kufunga shule walikuwa na changamoto hiyo.

"Hapa tulipofika  sasa ndio ameanza kutekeleza ahadi zake  hivyo tunamuomba Mhe. Diwani wakati mwingine atusaidie hata mabegi na sale za shule kwani hali wetu kifedha sio nzuri kutokana na changamoto mbalimbali za wazazi na walezi" amesema mmoja wa wazazi wa watoto  Fatuma Kaloli.

Amesema majukumu wake alitelekezwa na baba yake hivyo jukumu la kumlea analo yeye tangu anaanza chekechea hadi sasa yupo darasa la saba huku mama mzazi akiwa amepata changamoto ya ukiziwi.

Naye mzazi mwingine Tabu Adamu, alitoa pongezi kwa msaada huo na kuwa ni wakati mwafaka  kwa wadau wengine kuona umuhimu wa kujitokeza kuwasaidia watoto wasiokuwa na uwezo wa vifaa hivyo vya shule na si kumwachia Diwani peke yake.

Diwani Lyoto akizungumza na waandishi wa habari, alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kutokana na kwamba alipata taarifa ya kuwepo na watoto wenye uhitaji wa vifaa hivyo kutokana na wazazi wao kutokuwa na kipato cha kujitosheleza kwani wengi hasa akina mama walimfuata na kumwelewa kuwa wana changamoto hiyo kwa ajiri ya watoto wao.

Amesema mwezi  Januari alikuwa anafuatwa na wazazi na walezi kuomba msaada na ndipo akamua kuanzisha utoaji wa vifaa kupitia shule.

Lyoto amesema  japokuwa nimepata taarifa kumbe kuna watoto wengine hawana hata mabegi wala sale za shule na kuahidi kushughulikia.

"Masuala yote nimeyachukua kutokana na kwamba huu ndio mwanzo lakini pia kuna mfuko wa Diwani (Diwani Fund), ambao unaanzishwa mda si mrefu ambapo wafanyabiashara ndogo ndogo watakuwa wanakopeshwa bila riba lengo likiwa ni kuwafanya wajikwamue na umaskini lakini pia mwisho wa siku waache kuwa tegemezi," alisema.

Watoto waliopewa msaada huo wapo yatima, wasiokuwa na wazazi na wale waliotelekezwa ambapo pia Diwani huyo alisema kuwa watoto hao kwa Kata nzima kwa uchache huo  ataendelea kutoa msaada zaidi ili kuhakikisha wanafikiwa wote kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa pamoja na wadau wengine huku suala la chakula mashuleni likiendelea kufanyiwa kazi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...