MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amefanya ziara ya kutembelea Idara ya Mazingira ili kujua changamoto na kuangalia namna ya utendaji kazi sambamba na kubadilishana mawazo na watendaji hao juu ya namna bora ya kufikia malengo ya Serikali juu ya kuweka mazingira safi na salama.

Maalim Seif amekwenda katika ofisi hiyo iliyopo Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini magharib Unguja nakupokelewa na Wakurugenzi wa ofisi hio wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mjini  Rashid Simai Msaraka.

Idara ya Mazingira ni miongoni mwa Idara ambazo zipo chini ya Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Akielezea ripoti ya utendaji kazi wa ofisi Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa Mazingira  Sheha Mjaja Juma amesema mpaka sasa wameweza kudhibiti uwepo wa mifuko ya plastiki, mifuko ambayo  kwa kiasi kikubwa ilikua ikichafua mazingira.

Pamoja na hayo Mkurugenzi Rashid amesema kwasasa jamii imeanza kuwaelewa na kutambua umuhimu wa kutunza mazingira kwani walikuwa wanakutana na Changamoto nyingi walipokuwa wanatoa elimu ya mazingira kwa jamii.

Rashid ameleza kwamba wamefanikiwa kuanzisha jaa kubwa la kutupa takataka maeneo ya Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.

Katika Changamoto zao wamesema wanakutana na wakati mgumu wanapokuwa wanafanya ulinzi wa Maliasili zisizo rejesheka kama vile Mchanga,kifusi na kokoto kwani maranyingi wanakutana na mapambano na Wananchi ambao wanachukua vitu hivo bila ya kufata utaraibu.

Mkurugenzi amesema mbali ya kwamba tayari wamepata eneo la kutupa takataka hizo ila huko Kibele ila bado hawajafanikiwa kupata vifaa sahihi kwaajili ya kuchomea takataka hizo na badala yake wanazichoma katika hali ya kawaida.

Naye mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja  Mh. Msaraka amesema  katika kuondoa tatizo la takataka  katika Wilaya ya Mjini tayari Ofisi yake imeshaanza kufanya mazungumzo na makampuni kadhaa kutoka Nchi ya China, Qatar na Dubai ili kuona ni namna gani wataweza kuzibadilisha takakata kuwa mbolea lakini pia kuzibadilisha kuwa chakula cha samaki na kuku.

Msaraka amesema kwasasa suala la usafi katika Wilaya ya Mjini wamelikabidhi katika kampuni ya Green West ambayo wameingia nayo mkataba kuhakikisha jiji linakuwa katika hali ya usafi zaidi kwani mjini kuna mchanganyiko wa watu wengi wakiwemo watalii, jambo ambalo litaleta manufaa pia.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema ’’Sisi Serikali hatuwezi kulipuuza suala la Mazingira kwani suala la kutunza mazingira ni muhimu sana hata kwa afya zetu.’’

Maalim ameipongeza Idara hio kwa kuweza kupambana kwa kiasi kikubwa kuondoa matumizi ya mifuko ya plastiki lakini amewataka wafanyakazi wa Idara hio kwa kusaidiana na Serikali kwa ujumla kuangalia ni namna gani wataweza kuzalisha malighafi za ujenzi.  

Katika kusisitiza hilo Maalim amesema;

‘’Niukweli usiofichika kwamba kuchimba mchanga na mawe inaathiri mazingira, lakini kila siku watu wanajenga majumba na wanahitaji bidhaa hizo, sasa kaeni na Watafiti muangalie ni namna gani mutazalisha nyenzo nyengine za ujenzi mbadala wa kuchimba Mchanga na hayo mawe ili Wananchi pia waendelee na shughuli zao za ujenzi.’’ Amesema.

Maalim Seif alimalizia kwa kuwapongeza sana kwa  utendaji wao kazi japo kama licha ya kuwa na mazingira magumu ya ufinyu wa ofisi, na kuwaambia wajitahidi sana kufanya tathmini zaid pamoja na kutoa   ushauri katika namna za kutatua changamoto za kimazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...