Timu ya Mtwivila City (Ifuenga) wakishangila ushindi baada ya kutinga hatua ya fainali mara baada ya kuifunga timu ya Irole fc kwa jumla ya goli mbili moja.
mwenyekiti
wa umoja wa vijina wa chama cha mapinduzi (CCM) Makala Mapessa akiwa na
kocha wa timu ya Mtwivila City (Ifuenga) baada ya mechi ya nusu fainali
na kuingia fainali
Mwenyekiti
wa umoja wa vijina wa chama cha mapinduzi (CCM) Makala Mapessa
akifuatilia mchezo wa nusu fainali ya ligi ya mkoa wa Iringa kati ya
Ifuenga United na Irole fc uliochezwa katika chuo cha Mkwawa
Na Fredy mgunda,Iringa.
Mwenyekiti wa vijana wilaya ya Iringa vijijini amezipongeza timu zote
zilizoshiriki ligi ya mpira wa miguu mkoa wa Iringa (Asas super league)
kwa kuonesha uwezo mkubwa wa kuchezea kabumbu kwa kuwa na na wachezaji
wengi wenye vipaji vya hali ya juu kwa ngazi ya mkoa hadi kimataifa.
Akizungumza
mara baada ya mchezo baina ya Mtwivila city dhidi Irole Fc uliomalika
kwa timu ya Ifuenga United kutinga hatua ya fainali mara baada ya kuwafunga
timu ya Irole Fc kwa jumla ya goli mbili moja katika uwanja wa chuo
kikuu kishiriki cha Mkwawa,mwenyekiti wa umoja wa vijina wa chama cha mapinduzi (CCM) Makala Mapessa alisema kuwa halmashauri ya
wilaya ya Iringa vijijini imekuwa na timu bora kila mwaka ndio maana
kila mwaka lazima kwenye nusu fainali au fainali kuwe na Timu inayotoka
halmashauri hiyo.
Alisema
kuwa umoja wa vijan wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa umekuwa
ukitoa ushirikiano wa asilimia 100 kwa timu zote ambaozo zimekuwa
zinashiriki mashindano yoyote yale kwa kujua thamani ya vipaji vya
wachezaji wa mpira wa miguu katika wilaya hiyo.
Mapessa
aliwapongeza wadau wote ambao wamekuwa wakisaidia kukuza vipaji na Timu
zote za kutoka wilaya hiyo katika mashindano mbalimbali ambayo wamekuwa
wakishiriki kwa namna moja au nyingine.
"Moja
kati ya wilaya yenye vijana wenye vipaji mkoani Iringa ni wilaya ya
Iringa vijijini ambayo imekuwa ikitoa timu nyingi bora kwenye mashindano
mbalimbali mkoani Iringa"alisema
Akizungumzia
fainali ya Asas super league alisema kuwa ubingwa wa ligi hiyo lazima
ubaki katika timu ya Mtwivila city (Ifuenga) kwa kuwa timu hiyo
inawachezaji wengi wazuri ambayo wanaweza kushinda na timu yoyote ile
kutokana na ubora walio nao.
Mapessa alisema kuwa Mtwivila
city (Ifuenga) inauwezo wa kuifunga timu yoyote ile ambayo itakuwa
inashiriki mashindano au ligi ambayo timu hiyo inashiriki kwa ajili ya
ubora ambao wachezaji wake wanao kwa sasa.
Alimazia
kwa kuwataka viongozi wote kuhakikisha wanashinda ubingwa wa ligi ya
mkoa wa Iringa (Asas super league) kwa namna yoyote ile kwa kuwa timu
hiyo ina wachezaji wenye ubora na wanavipaji vya kushiriki mashindano
mbalimbali mkoani Iringa na nje ya mkoa wa Iringa.
Ikumbukwe kuwa Bingwa
wa ligi hiyo iliyojizoelea umaarufu nchini kutokana na udhamini wa
kampuni ya maziwa ya Asas ataondoka na sh milioni 2.5 huku mshindi wa
pili akichukua milioni 1.5 na mshindi wa tatu ataibuka na laki 750000
baada ya zawadi kuongezwa kwa washindi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...