NA  YEREMIAS  NGERANGERA..NAMTUMBO.

Mwenyekiti mpya  wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma  Juma  Pandu  amewataka  watumishi  wa  serikali katika  halmashauri ya wilaya ya Namtumbo  kuwajibika  ipasavyo  katika nafasi  zao  na kuongeza  ushirikiano katika  kazi.

Pandu  aliyasema hayo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa  Halmashauri hiyo  akiwa na wakuu  wa idara na vitengo  kueleza  changamoto  alizozibaini  katika ziara yake  ya kukagua  miradi katika Halmashauri hiyo  na kuwataka  watumishi kuwajibika katika nafasi zao  na kuongeza ushirikiano ili kuyapatia ufumbuzi  matatizo yanayoikabili  jamii .

Aidha  bwana  Pandu  aliwaambia  wakuu wa idara na vitengo anapenda kuona  ushirikiano kutoka kwa wakuu wa idara na vitengo  pamoja na waheshimiwa  madiwani  kwa kufanya hivyo  wataweza  kutatua changamoto  zilizopo katika jamii kwa  pamoja.

Alitaja  changamoto  ya  uhaba wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya ,watumishi  wachache  wa idara ya afya  na kumwagiza  mkuu wa idara ya afya  kuhakikisha  dawa zinapatikana  kwa wakati  na huduma  zitolewa  nzuri  kwa wagonjwa  alisema  bwana Pandu.

Changamoto  ya ujenzi wa  maboma  kwa nguvu za  wananchi  wenyewe  kama madarasa,vyoo,zahanati, bwana  pandu  alimtaka mkurugenzi wa Halmashauri  kuhakikisha  wataalamu  wanafika katika maeneo  yanakojengwa  maboma hayo  ili majengo yanayojengwa yawe na ubora  wa kiwango cha serikali.

Diwani  wa kata  ya  Limamu  bwana  Isdori  Nyati  katika kikao hicho alidai ucheleweshaji  wa utoaji wa  fedha  kwa wajumbe  kutoka vijijini  unachukua muda mrefu  na kutaka swala hilo  liwekewe  utaratibu  ili kupunguza  kero kwa  wananchi wanaofuata  huduma za kuchukua  fedha.

Mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri  ya wilaya ya Namtumbo  Evance  Nachimbinya  pamoja na kuwashukuru  wajumbe  wa kikao hicho alisema wamepokea  maagizo hayo  na kwenda  kuyafanyia kazi lakini  utaratibu wa utoaji wa fedha za serikali  utazingatia sheria, kanuni  na taratibu zilizowekwa  na sio vinginevyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...