Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba na Mkurugenzi wa Shirika la Water Mission Tanzania, Benjamin Filskov wakikata utepe kuzindua mradi mpya wa maji wa Ikombo uliopo Wilaya ya Chamwino, Dodoma.Mradi huo utahudumia wananchi wapatao 4,172 pamoja na taasisi za kijamii kama shule, kliniki pamoja na masoko.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba na Mkurugenzi wa Shirika la Water Mission Tanzania, Benjamin Filskov wakinywa maji safi kutoka kwenye mradi mpya wa maji wa Ikombo uliopo Wilaya ya Chamwino, Dodoma.Mradi huo utahudumia wananchi wapatao 4,172 pamoja na taasisi za kijamii kama shule, kliniki pamoja na masoko.

 

========  =======  ======  =====

·        Mradi huo utatoa maji safi na salama kwa wananchi wapatao 4,172.

 Dodoma. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba amelipongeza Shirika la Water Mission Tanzania kwa kufanikisha ujenzi wa mradi wa maji wa Ikombo Wilayani Chamwino ambao utasaidia kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wapatao 4,172.

 Mradi huo wenye thamani ya Shilingi 300 milioni umejengwa kwa ushirkiano kati ya Shirika hilo, Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) na wananchi na utasaidia kupunguza adha ya maji kwa zaidi ya asilimia 97. Pia, utasaidia kutoa huduma kwenye kliniki, hospitali pamoja na shule kwenye eneo hilo.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Nadhifa Kemikimba ambaye alimwakilisha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, alisema mradi huo ni sehemu ya miradi mingi ya maji vijijini yenye lengo la kuhakikisha hadi ifikapo mwaka 2025 wananchi wanapata huduma ya maji kwa asilimia 95.

 Mhandisi Kemikimba alisema lengo la mradi huo ni kuwapatia wananchi wa Ikombo maji safi na salama karibu na makazi yao ili kuwapunguzia adha na muda wa kutembea umbali mrefu badala ya kufanya shughuli zingine za maendeleo.

 “Utaratibu ni kwamba kila baada ya mita 400 kuwe na bomba la maji safi na salama na ndani ya nusu saa mwananchi awe ameteka maji na kuondoka."

 Mhandisi Kemikimba alilishukuru Shirika la Water Mission kwa msaada mkubwa walioutoa kugharamia mradi huo muhimu na kuahidi Serikali na wananchi kuuenddeleza mradi huo.

 Aliongeza "Nawashukuru Shirika la Water Mission kwa msaada mkubwa mlioutoa kugharamia mradi huu muhimu, naahidi Serikali na wananchi tutaulinda ili udumu zaidi ya miaka mingi zaidi ili vizazi vilivyopo na vijavyo viweze kunufaika na mradi huu,” alisema.

 Mkurugenzi wa Water Mission, Benjamin Filskov, alianza kwa kupongeza ushirikiano kati ya Water Mission, wanakijiji wa Ikombo na RUWASA kwa  kufanikisha ujenzi wa mradi huo.

 Alisema kinachotakiwa ni uendelezaji wa muda mrefu wa mradi huo wa Ikombo, Kulinda miundombinu, na kusimamia vizuri mapato ili kamati ya maji iwe na uwezo wa kutengeneza palipoharibika.

 Alisema juhudi hizo zimefanikisha kukamilika kwa mradi wenye uwezo wa kujiendesha na wa muda mrefu utakaosaidia kutoa huduma ya maji kwa wakazi wa eneo hilo.

 “Lengo letu ni kushirikiana na kuwa mshirika muhimu katika utekelezaji wa miradi ya maji.Leo hii tunafarijika kufungua mradi huu mbao utaondoa uhaba wa maji kwa wakazi wa eneo hili.Mafanikio haya yanadhihirisha ushirikiano baina ya RUWASA wananchi pamoja na Wizara ya Maji,” alisema.

 Wananchi wa eneo hilo waliahidi kulinda kwa kila hali miundombinu ya mradi huo ili udumu kwa muda mrefu lakini pia kusambaza huduma hiyo katika vitongoji vingine vya kijiji hicho ambavyo ni Juhudi na Chapakazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...