Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mkoani Mara  imewahukumu watu 6 kunyongwa hadi kufa kwa kosa la Kuuwa watu 17  wa familia Moja.

Akisoma hukumu hiyo Januari  15, 2021 mbele ya Mheshimiwa Jaji Mustapha Siyani katika Kesi ya Jinai Na. 56 ya Mwaka 2018  Jamhuri dhidi ya Juma Mugaya na wenzake 8, katika Kesi  ya mauaji ya watu 17 maarufu kama kesi ya Mugaranjabo, imewatia hatiani washtakiwa sita na kuwapa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa makosa yote 17 ya kuua watu wa familia moja ili kulipiza kisasi kutokana na ndugu yao Fred Mugaya kuuawa na wananchi kwa tuhuma za wizi wa mifugo.

Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo  tarehe 16 februari 2010, katika eneo la Mugaranjambo lililopo Musoma Mkoa wa Mara ili kulipiza kisasi kwa kuwaua watu 17 wa familia moja kama sehemu ya kulipiza kisasi kutokana na ndugu yao Marehemu Fredy Mugaya kuuawa na wananchi wa Mgaranjambo mwaka 2005 kwa tuhuma za wizi wa mifugo,  baada ya mzee wa familia hiyo Marehemu Kawawa Kinguye kupiga yowe wakati wizi wa mifugo unafanyika nyumbani kwake hivyo baada ya tukio hilo washitakiwa walipanga.kulipa kisasi.

Hivyo  siku ya tukio walitekeleza kwa kuwakata kata  kwa mapanga na kuwauwa watu kumi na Saba(17) wa familia moja huku wengine watatu wakiwaacha na vilema vya kudumu.

Awali kesi hiyo  ilikuwa na washtakiwa kumi na sita  lakini wengine walifariki vifo vya kawaida wakiwa Magereza kabla ya  kesi kusikilizwa.

 Akitoa hukumu hiyo  Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa  Mustapha Siyani aliwatia hatiani washitakiwa sita  na kutoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa  na kuwaachia huru washitakiwa watatu.

Washtakiwa waliotiwa hatiani ni Juma Mugaya,Aloyce Nyabasi, Nyakaranga Wambura Biraso, Nyakaranga Masemere Mugaya, Sadock Alphonce  Ikaka na Kumbasa Buruai Bwire na walioachiwa huru ni Marwa Maua Mugaya, Ngoso Mgendi Ngoso na Sura Bukaba Sura

Kesi hiyo  iliendeshwa na Mawakili wa Serikali, Renatus Mkude, Valence Mayenga,  Robert Kidando,  Ignatus Mwinuka na Yese Temba ambapo upande wa utetezi uliwakilishwa na Mawakili tisa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...