Na Mwandishi wetu, Simanjiro
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Manyara, imeanzisha
mpango wa kusikiliza kero za wananchi kwa kuwafuata vijijini kupitia
ofisi inayotembea (mobile office) ili waweze kuwafikia kwa wingi zaidi.
Mkuu
wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Makungu aliyasema hayo jana wakati
akizungumza na wananchi wa kata ya Naisinyai wilayani Simanjiro.
Makungu
amesema kwa kuanzia wamefikia kijiji cha Naisinyai na kusikiliza kero
na changamoto mbalimbali za wananchi Kisha wataendelea na vijiji vingine
vya mkoa wa Manyara.
"TAKUKURU
tumeona hakuna haya ya kukaa ofisini ila kupitia mobile ofisi tutaweza
kuwafikia wananchi wengi zaidi na kusuluhisha changamoto zilizopo na
kufuatilia nyingine kwa ukaribu zaidi," amesema Makungu.
Amewataka
wakazi wa eneo hilo kutoa kero, changamoto na matatizo yao bila hofu
yoyote kwani hakuna mtu au kiongozi ambaye atawahoji baada ya
kuwasilisha hoja zao.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Naisinyai, Merika Makeseni amesema wananchi wa eneo hilo
wanaamini katika mazungumzo na siyo kulalamika pindi wakiwa na kero zao.
"Tuna
matumaini kuwa kero mbalimbali zilizofikishwa na wananchi kupitia
TAKUKURU zitafanyiwa kazi na kupatikana ufumbuzi wake," amesema
Makeseni.
Amesema
wanawakaribisha tena TAKUKURU baada ya miezi sita au mwaka mmoja warudi
na majibu ya ufumbuzi wa kero mbalimbali za wananchi zilizotolewa kwenye
mkutano huo wa TAKUKURU inayotembea.
Mkazi
wa kijiji cha Naisinyai John Mollel amesema wamehitimu mafunzo ya
mgambo tangu mwaka 2017 ila hawajapatiwa vitambukisho na vyetu vya
kuhitimu.
Mkazi mwingine
Isack amesema baadhi ya askari wanaolinda ukuta unaozunguka machimbo ya
madini ya Tanzanite wanawapiga raia na kunyan'ganyana wanawake wao.
Mkazi
mwingine Aloyce Kiroia amesema kuna kigogo mmoja anafanya utaratibu wa
kuchukua ardhi ya kijiji hicho hivyo achukuliwe hatua kali.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara Holle Joseph Makungu
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro
kwenye mkutano wa kuwajengea uwezo juu ya rushwa na kusikiliza kero
mbalimbali kupitia ofisi ya TAKUKURU inayotembea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...