Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari.
………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, Babati
TAASISI ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Manyara, imeandaa mpango kazi wake
utakaotekelezwa kwa muda wa miezi mitatu ya kuanzia Januari hadi Machi
mwaka huu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu ameyasema hayo mjini Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Makungu amesema
miongoni mwa mpango kazi wao ni kujikita zaidi kwenye kudhibiti miradi
ya maendeleo, udhibiti wa madini ya Tanzanite kuhakikisha kanuni za
usafirishaji wa madini za mwaka 2019 zinafuatwa.
Amesema pia
watafuatilia ukopeshaji wa matrekta yaliyotolewa na shirika la maendeleo
la Taifa (NDC) ilikuhakikisha fedha zinarejeshwa na wakulima zaidi
wanakopeshwa kupitia fedha hizo.
Amesema watafuatilia
pia mikopo ya matrekta toka TIB DEVELOPMENT LIMITED wanawataka waliokopa
wafike TAKUKURU baada ya taarifa kutolewa ili wapewe utaratibu wa namna
ya kurudisha mikopo hiyo kwa mujibu wa mikataba yao.
“Kwa watakaokaidi
watalazimishwa ili mikopo hiyo iwezwe kuwanufaisha pia wakulima wa nchi
hii hatimaye tuweze kuondokana na jembe la mkono ambalo tija yake ni
kidogo kwa maana ya kilimo tulichokusudia kifanywe na wananchi wetu,”
amesema Makungu.
Amesema pia kwenye
kipindi hicho watafuatilia hujuma zinazofanywa kwa wakala wa ufundi wa
umeme TEMESA kwa maofisa maduhuli kukataa kulipa madeni ya fedha za
matengenezo hivyo TEMESA kushindwa kufanya kazi zake ipasavyo na
kushindwa kununua vipuri hivyo hupeleka magari kwenye karakana binafsi.
“Mfano ofisi fulani
jina linahifadhiwa ambayo kwa mujibu wa kumbukumbu za TEMESA inadaiwa
shilingi 89, 591, 175, 39 hayo ni matumizi mabaya ya madaraka, tunatoa
hadi Februari 28 mwaka huu wadaiwa wote wa TEMESA Manyara wawe wamelipa
na tutaanza uchunguzi kwa maofisa hao wasiolipa tutawachukulia hatua na
majina yao tutaweka hadharani,” amesema Makungu.
“Jambo la mwisho
ninalotaka wananchi wa mkoa wa Manyara kufahamu ni kuwa tumeanzisha
ofisi ya TAKUKURU inayotembea kwa kutenga siku moja kila mwezi na
kuwatembelea kwa kuwafuata wananchi mahali walipo na kusikiliza kero zao
na kuzitatua,” amesema Makungu.
Amesema kwa kuanzia
Januari 18 mwaka huu waliotembelea eneo la kijiji cha Naisinyai Mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro na kusikiliza kero mbalimbali za
wananchi na kuzitatua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...