KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Tigo Tanzania, leo imezindua tena huduma ya malipo.
Huduma hiyo ya malipo awali ilitambulishwa mwaka 2014 kwa jina la 'Lipa Hapa kwa Tigo Pesa' ili kuwafanya wateja kununua bidhaa mbalimbali kwa njia ya kidijitali.

Kwa sasa huduma hiyo imepewa jina la 'Lipa kwa Simu' ambapo imekuja ikiwa ineboreshwa zaidi na kwamba mteja atatumia kufanya malipo mbalimbali bila kutumia namba za QR na zingine katika kupata huduma.

'Lipa kwa Simu' ni huduma ya kifedha ya kidijitali inayomfanya mfanyabiashara au taasisi kupokea fedha kutoka wateja wanaotumia simu za mkononi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo Cha Fedha Cha Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema: “Soko la ndani lina sifa ya ukuaji mkubwa kwa idadi ya watu, idadi ya vijana na viwango vya juu vya data na kupitishwa kwa njia ya kidijitali.

 "Madhumuni yetu ni kutanua na kuboresha njia zote za malipo nchini Tanzania. Tunaamini, huduma mpya ya Lipa kwa Simu, itawapa wateja wote wa Tigo Pesa pamoja na watumiaji wengine wa pesa, uzoefu mkubwa wa malipo kwa kuwawezesha kufanya shughuli zao zote za malipo kwa njia salama na rahisi”.

“Pamoja na kuletwa kwa namba za QR na namba zingine katika Lipa kwa Simu tumejipanga kuleta ubunifu na usanifu kwa shughuli za Tigo Pesa.

"Kwa wafanyabiashara, tunaanzisha uzoefu wa ndani ya programu ambapo wataweza kusimamia ushuru wao wa malipo kupitia App ya Tigo Pesa, hii itaruhusu urahisi na udhibiti zaidi wa fedha za  biashara," alisema.

Uzinduzi huu pia unaenda sambamba na spesho promosheni ambayo itakua ni kwa ajili ya wateja wote wakipata ongezeko la fedha kila watakapotumia huduma ya 'Lipa Kwa Simu'.

Alisema huduma hiyo itakua inapatikana katika maeneo mbalimbali ikiwemo sokoni, sheli za mafuta, cinema, sehemu za vyakula, hotelini, wanapouza vinywaji, supermarket, maduka ya madawa na wanapouza vifaa vya ujenzi.

Alisema kuwa huduma hiyo itatumia kwa wateja wote wa Tigo Pesa na haina haja ya kujisajili.

Wateja wote wanatakiwa kufanya kifuatacho:
1.Bonyeza *150*01#
2.Chagua ‘5’ Lipa Kwa Simu, alafu
3.Chagua “1” kwa Tigo Pesa au unaweza kulipa kwa kutumia Tigo Pesa App na kufurahia huduma hiyo ambayo ni rahisi.



Huduma hii ya malipo, sasa itafahamika kama Lipa kwa Simu, na tunaizindua leo hapa sokoni Kariakoo, ili wafanya biashara waweze kuielewa huduma hii, na pia waanze kuitumia kwani ni rahisi na salama. Angelica Pesha-Mkuu kitengo cha Tigo Pesa
Kama kampuni ya kidigitali siku zote tunalenga kuleta suluhisho na kufanya maisha ya wateja wetu kuwa rahisi zaidi na ndio mana leo tunazindua huduma hii maalumu kwa wateja na wafanyabiashara wote”.Reuben Kamuga-Meneja wa huduma Lipa kwa Simu.

Lipia usafiri wa boda boda kwa kutumia malipo kwa njia ya Simu #LipaKwaSimu #TigoPesa #Uzinduzi

Ukinunua chochote kwa wafanyabiashara waliojisajili na Lipa kwa simu maliza malipo yako kirahisi na Lipa Kwa Simu.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...