Na.Vero Ignatus.

Kasi ya kusafirisha nyama kwenda nje ya nchi imeongezeka kutokana na kuwepo kwa ubora wa Viwanda vya nyama, ikiwa ni uwekezaji mkubwa uliopo jambo linalosababisha kuwepo kwa nyama bora, na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na kukidhi soko la ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania ,Imani Sichalwe akiwa kwenye ziara ya kukagua mazingira ya usafirishaji wa nyama, kutoka Tanzania kwenda nchi za nje ,aliyoifanya  januari 2021 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere Jijini Dar es salaam.

Sichalwe alisema kuwa uwepo wa viwanda hivyo vya nyama vya kisasa  Nchini , ndio vinafanya kuwe na ithibati ya kupeleka nyama nje ya nchi,ambapo kiwanda Cha Tanchoice kilichopo Kijiji cha soga wilayani Kibaha Mkoani Pwani ,chenye uwezo wa kuchinja mbuzi 4500 kwa siku, na ng'ombe 1000 kwa siku moja ,ambapo kwa Tarehe 16.01.2021 kimepeleka mbuzi 2000 waliochinjwa Sawa na kilo 20,000 au tani 20 kwenda Oman na Kuwait.

"Kwa Sasa kwa wiki kiwanda cha nyama cha Tanchoice kilichopo Kibaha Mkoani Pwani husafirishwa mbuzi waliochinjwa 6000 sawa na kilo 60,000 sawa na tani 60 kwenda Omani,Qatar na Kuwait na kwa wiki ijayo kiwanda kitaanza kupeleka nyama katika soko jipya la Hongkong. Kwa upande wa kiwanda Cha Nyama Cha Eliya Foods Overseas Limited kimeanza kupeleka nyama kwenda Oman Mbuzi 1874 sawa na tani 14.6" amesema Sichalwe.

Katika ziara hiyo ya kukagua mazingira ya usafirishaji wa nyama kwenda nje ya nchi Kaimu msajili Bodi ya Tanzania amesema ameridhika na namna shughuli nzima ya utaratibu unaofanywa kuanzia kushusha nyama kwenye gari,kuingiza kwenye vyumba maalumu vya kuhifadhia nakupooza pamoja na namna ya upakiaji wa nyama hizo kwenye ndege.

Muonekano wa Nyama ya mbuzi ikiwa kwenye kifaa maalumu Cha kuhifadhia nyama kabla  ya kupakiwa kwenye ndege Tayari kusafirishwa nje ya nchi.
Kaimu Msajili bodi ya nyama Tanzania Imani Sichalwe Mwenye suti kulia akipata maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa kupakia mizigo kwenye ndege namna utendaji kazi wao unavyoendelea kwa kuzingatia usalama na afya kwa mlaji wa Nyama katika zoezi la kupakia Nyama kwenda nje ya nchi.
Kaimu Msajili bodi ya nyama Tanzania Imani Sichalwe wa tatu kutoka kulia (Mwenye suti) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa mwalimu Julias Kambarage Nyerere wakati wa ziara ya ukaguzi wa usalama wa nyama inayosafirishwa kwenda nje ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...