Na Linda Shebby Kibaha
MENEJA wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (DAWASA ) Mkoa wa Kibaha Alfa Amos Ambokile amesema kuwa mradi wa maji katika eneo la Pangani uko kwenye hatua za mwisho huku akisisitiza kuwa utekelezwaji wakw umepangwa kufanyika katika kipindi cha mwaka mpa wa fedha utakao anza baadaye mwaka huu.
Meneja huyo alisema hayo kufuatia kuulizwa na wakaazi wa eneo la Pangani ambao wamekua wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji kwa muda mrefu sasa.
Alisema eneo la Disunyala nalo tayari michoro yake imekamilika katika mradi wa kimkakati hivyo nao litashughulikiwa katika mwaka wa fedha wa utekelezaji baadaye mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi zao zilizopo Wilayani Kibaha Ambokile amesema kuwa
"kwa maelezo mafupi naweza kusema kuwa hadi sasa tayari miradi ambayo tayari imekamilika ni pamoja na Mradi wa maji Soga ambao umekamilika kwa asilimia 100 (100%)ambapo wananchi tayari wameshaanza kupata huduma ya maji."
Aidha alitaja maeneo mengine ambayo ambayo kazi zinaendelea ni pamoja na Mbwawa ambapo mradi umekamilika kwa asilimia 80 (80%), alisema kuwa katika eneo hili zimebaki maeneo machache huku akisisitiza kwamba mafundi wako katika eneo husika wakiendelea na kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...