Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewataka Viongozi ngazi Mitaa kuhakikisha wanashughulikia ipasavyo kero na changamoto mbalimbali kwenye mitaa yao na kuhakikisha wanatoa taarifa mapema pale wanapobaini Jambo lipo juu ya uwezo wao ili liwezekushughulikiwa na ngazi za juu.

RC Kunenge amesema hayo wakati wa kikao chake na Watendaji na Wenyeviti wa mitaa Jijini humo ambapo amesema ni Jambo la fedhea kuona kiongozi wa ngazi ya juu anashughulikia kero ya mtaa wakati wahusika wa ngazi ya mtaa wapo wanapeta.

Aidha RC Kunenge amewaelekeza Watendaji wa Mkoa huo kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ukusanyaji wa Mapato ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya Mapato, kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ambapo amesisitiza ukusanyaji wa Mapato usiwe wa kero Wala wa kuua Biashara za watu.

Hata hivyo RC Kunenge amewataka Viongozi wa Mitaa kusimamia ipasavyo suala la usafi wa mazingira kwenye mitaa yao ili kuwakinga wananchi na magonjwa ya Mlipuko.

Pamoja na hayo RC Kunenge amewasisitiza pia Viongozi hao kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa watu wanaohatarisha usalama ikiwemo kufichua nyumba zinazogeuzwa Madanguro, wanaowahifadhi wahamiaji haramu, wanaowatumia walemavu kujinufaisha na wauzaji wa dawa za kulevya.

Sanjari na hayo amezielekeza Taasisi za umma zilizopo jiji humo kuhakikisha wanashirikiana na Watendaji wa Mitaa kwakuwa hao ndio wapo karibu na wananchi na ndio wanaozijua zaidi kero za mtaa yao.

Mkutano huo baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Viongozi mbalimbali wa Mitaa umedhaminiwa na Bank ya CRDB chini ya Kauli mbiu isemayo "UWAJIBIKAJI WA PAMOJA NI CHACHU YA MAENDELEO YA MKOA WETU".






 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...